• HABARI MPYA

    Saturday, November 21, 2015

    CANNAVARO: WAZANZIBARI WAJIANDAE KUTUPOKEA NA KOMBE

    NAHODHA wa Zanzibar, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amewataka wapenzi wa soka visiwani humo kujiandaa kupokea na kushangilia Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwezi ujao.
    Cannavaro amesema kwamba uteuzi wa kikosi cha Zanzibar cha Challenge mwaka huu ni mzuri mno na anaamini wanachukua Kombe.
    “Sisi wachezaji tunajuana, kwa kweli hiki kikosi ambacho kimekuja Challenge ni kizuri sana na tuna uwezo wa kuchukua Kombe na hiyo ndiyo dhamira yetu,”amesema.
    Nahodha wa Zanzibar, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema wamekwenda Addis kuchukua Kombe

    Beki huyo wa Yanga SC amesema kwamba wachezaji wote wa Zanzibar wamekubaliana kupigana kufa na kupona kuhakikisha wanabeba Kombe hilo.
    CECAFA Challenge inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo nchini Ethiopia wenyeji wakifungua dimba na Rwanda mjini Addis Ababa.
    Mchezo huo wa Kundi A utatanguliwa na mechi nyingine ya Kundi B, kati ya Burundi na Zanzibar.
    Tanzania Bara watatupa kete yao ya kwanza kesho, watakapomenyana na Somalia katika mchezo wa Kundi A, wakati mabingwa watetezi, Kenya watasuguana na mabingwa wa kihistoria, Uganda baadaye. 
    Mechi za mzunguko wa kwanza wa makundi zitakamilishwa keshokutwa, Sudan Kusini wakimenyana na Djbouti kabla ya Sudan na Malawi kufuatia baadaye.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CANNAVARO: WAZANZIBARI WAJIANDAE KUTUPOKEA NA KOMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top