Na Samira Said, ZANZIBAR
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Grand Malt leo imekabnidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu 12 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Grand Malt visiwani humo vyenye thamani ya Sh, milioni 244.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, Said Ally Mbarouk, meneja wa kinywaji cha kinywaji cha Grand Malt, Consolatha Adam, alisema kuwa wanafurahi kuona udhamini wao umesaidia kukuza kiwango cha wachezaji wa soka wa Zanzibar.
Waziri wa habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh Said Ally Mbaruk akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Amani kwenye Dhifa ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa viongozi wa timu zote za Ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar. Kulia ni Rais wa ZFA Radhia Raina na kushoto ni meneja wa kinywaji cha Grandmalt Consolata Adam
Meneja huyo alisema kuwa TBL inawashukuru wadau wote wa michezo wa Zanzibar kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi cha miaka mitatu waliyodhamini ligi hiyo inayotoa wawakilishi kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.
Alisema kuwa udhamini wao mwaka huu wameuboresha kutoka Sh. Milioni 204 msimu uliopita na kufikia Sh. Milioni 244 msimu ujao ambao unatarajiwa kufanyika kuanzia mapema mwezi Agosti mwaka huu.
Akipokea vifaa hivyo, Wazir Mbarouk, alisema kuwa udhamini wa Grand Malt umewasaidia kukuza soka la Zanzibar na hali hiyo imeonekana kwa wachezaji wake kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa idadi kubwa tofauti na miaka ya nyuma.
Waziri huyo alisema pia jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kupata wadhamini washiriki ambao watasaidia kutoa Fedha na hatimaye klabu zinazoshiriki kupata donge nono .
“Pia maoni ya kutaka timu katika ligi hii ziongezeke tumeshayapokea na tunayafanyia kazi, nimefurahi pia kuona mwaka huu kilio cha viatu kwa wachezaji kimefanyiwa kazi,” alisema Waziri huyo.
Meneja wa kinywaji cha Grandmalt Consolata Adam akimkabidhi vifaa vya Michezo kwa timu zaa ligi kuu ya Zanzibar kwa Waziri wa habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh Said Ally Mbaruk.
Naye Rais wa Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA), Razia Raina, aliishukuru Grand Malt kwa udhamini wake na wanawaomba waendelee tena kuidhamini ligi hiyo.
Alisema kwamba udhamini wao uliongeza ushindani kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.
Ligi ya Zanzibar inashirikisha timu 12 ambazo ni pamoja na bingwa mtetezi KMKM, Polisi, Mafunzo, Miembeni, Zimamoto, JKU, Kipanga, Chuoni, Malindi, Shaba, Hard Rock na Mtende Rangers.

.png)
0 comments:
Post a Comment