• HABARI MPYA

    Wednesday, July 09, 2014

    NICO KIONDO KOCHA MPYA SIMBA B

    NA Nagma Khalid, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya soka la vijana ya Simba imempa shavu mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Nico Kiondo kukinoa kikosi hicho cha Simba B kinachojiandaa na mashindano ya  Rollingstone.
    Kiondo aliyewahi kukinoa kikosi cha Ashanti United, akisaidiana na Abdallah Kibadeni kabda ya timu hiyo haijashuka daraja amepewa jukumu la kuinoa timu hiyo jana na kamati ya vijana iliyochini ya Mwenyekiti wake Said Tully.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Tully alisema timu yao itaingia kambini leo kwenye Chuo cha Ardhi Dar es Salaam kujiandaa na mashindano hayo.
    Nico Kiondo (katikati) ndye kocha mpya wa Simba B

    Alisema mashindano hayo kwa mwaka huu yanafanyika Dar es Salaam, kuanzia Julai 15 mwaka huu na itatumia viwanja vitatu vya Azam Complex, Karume na Bandari.
    “Mimi na kamati yangu tumeona timu ingie kambini mapema ya kujiandaa na mashindano hayo, ambapo watakuwa wanafanya mazoezi Chuo cha Ardhi,”alisema.
    Alisema kamati yake yenye viongozi imara Ally Suru, Patrick Rweyemamu, Mulamu Nghambi, Madaraka Suleiman na Amina Poyo imedhamiria kuchua ubingwa wa mashindano hayo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NICO KIONDO KOCHA MPYA SIMBA B Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top