NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anaendelea kujifariji baada ya kutolewa Kombe la Dunia kwa kula raha na mpenzi wake, Irina Shayk.
Akiwa ameshindwa kuisaidia Ureno iliyotolewa hatua ya makundi Kombe la Dunia nchini Brazil, ameposti picha akiwa na mpenzi wake Irina Shayk wake nje ya helikopta asubuhi ya leo wanajiandaa kupanda chombo hicho kwenda kwenye matanuzi.
Ronaldo ambaye wiki iliyopita aliposti picha akiwa na Irina, leo ameposti picha hiyo akiwa nje ya helikpota akiambatanisha na ujumbe usemao; 'safari asubuhi'.

Mapozi: Cristiano Ronaldo (kushoto) awali aliposti picha hii akiwa na 'mupenz', mwanamtindo wa Urusi, Irina Shayk kulia
Wakati Mwanasoka huyo Bora wa Dunia anakula bata, mpinzani wake mkubwa, nyota wa Barcelona, Lieonel Messi anaendelea kutesa uwanjani akiwa ameiwezesha Argentina kutinga Fainali Kombe la Dunia, baada ya kuitoa Uholanzi kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120.
Sasa Messi anaingia kwenye jaribio la kutwaa Kombe la kwanza la Dunia atakapoiongoza Argentina katika Fainali Jumapili dhidi ya Ujerumani.

Mambo uwanjani: Lionel Messi anaendelea kutesa katika Kombe la Dunia, wakati Ronaldo anajifariji kwa starehe



.png)
0 comments:
Post a Comment