• HABARI MPYA

    Friday, July 11, 2014

    HAPANA CHEZEA ARSENAL, BAADA YA KUMNASA SANCHEZ, WAPELEKA POSA YA KHEDIRA REAL MADRID

    KLABU ya Arsenal imebisha hodi Real Madrid kuulizia bei ya kiungo Sami Khedira. 
    Ikiwa imekwishamsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez kutoka Barcelona, The Gunners sasa inahamishia mawindo yake kwa kiungo huyo mkabaji wa Ujerumani. 
    Khedira, ambaye amebakiza miezi 12 katika Mkataba wake Real, yuko juu katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Arsene Wenger. 
    Anayepiga kichwa: Sami Khedira yupo kwenye dada za Arsenal, ambao wanaweza kutoa ofa ya Pauni Milioni 20
    Future team-mates? Mesut Ozil and Khedira in training on Thursday
    In action: The German against Brazil earlier this week
    Anaondoka: Khedira anaweza kucheza sambamba na Mesut Ozil (kulia) msimu ujao. Ujerumani imeingia Fainali ya Kombe la Dunia Brazil

    Klabu hiyo imeomba kujua bei ya Khedira na kuna uwezekano dili hilo likafanikiwa kwa sababu mchezaji huyo anaweza kuuzwa kwa bei ambayo Arsenal wataimudu.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaweza kuuzwa kwa Pauni Milioni 20, licha ya kwamba amebakiza miezi 12 ya kuishi Madrid.
    BIN ZUBEIRY inafahamu Khedira anataka mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki, kiasi ambacho kitamfanya awe mchezaji anayelipwa zakidi Arsenal.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAPANA CHEZEA ARSENAL, BAADA YA KUMNASA SANCHEZ, WAPELEKA POSA YA KHEDIRA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top