• HABARI MPYA

    Friday, July 11, 2014

    RASMI, SUAREZ NI KIFAA YA BARCELONA

    MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameondoka Liverpool rasmi akihamia Barcelona kwa dau la uhamisho la Pauni Milioni 75.
    Liverpool imekamilisha vipengele vya mkataba wa kuuza mchezaji kwa dau la rekodi katika klabu hiyo kwa Barcelona kumnunua mshambuliaji mkorofi, Luis Suarez.
    Hata hivyo, Suarez hatatambulishwa Uwanja wa Camp Nou kama ilivyo utamaduni wa klabu hiyo, kwa sababu amefungiwa miezi minne kujihusisha na soka baada ya kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini wakati wa Kombe la Dunia.  Amepewa jezi namba tisa.
    Dole tupu: Luis Suarez amekamilisha uhamisho wa Pauni  Milioni 75 kutua Barcelona kutoka Liverpoor
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RASMI, SUAREZ NI KIFAA YA BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top