• HABARI MPYA

    Friday, July 11, 2014

    HAYA NDIYO MAISHA YA FRANK DOMAYO KWA SASA, YEYE NA KITANDA, KITANDA NA YEYE

    Ataishi hapa kwa mwezi mzima, baada ya hapo atainuka kwenda kutoa hogo. Ataendelea kuugulia maumivu kwa miezi mitatu zaidi kabla ya kuanza mazoezi mepesi. Hiyo ni baada ya kiungo Frank Domayo kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja wiki iliyopita nchini Afrika Kusini, siku chache tangu ajiunge na Azam FC akitokea Yanga SC, zote za Dar es Salaam.
    Huyu ni kinda aliyeibukia vizuri msimu uliopita katika kikosi cha kwanza cha Azam, winga Joseph Kimwaga ambaye naye alifanyiwa upasuaji wa goti Afrika Kusini. Naye pia atakuwa nje kwa miezi minne. Wawili hawa wapo chumba kimoja, nambari 19, katika hosteli za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, makao makuu ya klabu ya Azam FC. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAYA NDIYO MAISHA YA FRANK DOMAYO KWA SASA, YEYE NA KITANDA, KITANDA NA YEYE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top