• HABARI MPYA

    Friday, March 13, 2020

    CAF YAFUTA MECHI ZA TAIFA STARS NA TUNISIA KUFUZU AFCON 2021 KWA SABABU YA CORONA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MECHI mbili za kufuzu Fainali za Kombe za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 baina ya Tanzania na Tunisia zilizokuwa zifanyike mwishoni mwa mwezi huu Tunis na Dar es Salaam zimeahirishwa.
    Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limesimamisha mechi zote za kufuzu za mashindano ya Afrika kwa ushauri wa Shirika la Afya Dunani (WHO) kufuatia mlipuko wa virusi COVID-19 hadi hapo itakapaoamuliwa vinginevyo.
    Mechi zilizofutwa ni za tatu za na za nne kufuzu Fainali za AFCON 2021 ambazo zilipangwa kufanyika kati ya Machi 25 na 31 mwaka huu, kufuzu Fainali za Kombe la Dunia la Wanawake chini ya umri wa miaka 20 zilizopangwa kufanyika kati ya Machi 20 na 22 na marudiano Machi 27 na 29 mwaka huu.
    Aidha, CAF pia imesitisha mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa (AFCON) kwa Wanawake 2020 zilizopangwa kufanyika kati ya Aprili 8 na 14 mwaka 2020 – na ratiba mpya ya michuano hiyo itatangazwa kwa wakati.
    Tayari kikosi cha timu ya taifa ya Tanzana kimeingia kambini tangu jana kujiandaa na mchezo wa Kundi J kufuzu AFCON dhidi ya Tunisia uliopangwa kufanyika Machi 27 Jijini Tunis na marudiano Machi 30 Dar es Salaam.
    Mpango wa kocha Mrundi, Ettiene Ndayiragije ni baada ya mechi hizo mbili za nyumbani na ugenini dhidi ya Tunsia kuwania tiketi ya AFCON, wachezaji wanaocheza nje waruhusiwe kurejea katika klabu zao na wanaocheza nyumbani wabaki kambini kujiandaa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zilizopangwa kufanyika Cameroon kuanzia Aprili 4 hadi 25, mwaka huu nchini Cameroon.
    Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo kinaundwa na makipa; Bakari Kissu (Gor Mahia - Kenya), Metacha Mnata (Yanga SC), Aishi Manula (Simba SC) na Salum Salula (Malindi FC).
    Mabeki ni; Shomari Kapombe (Simba SC), Juma Abdul (Yanga SC), Kelvin Kijiri (KMC), Mohamed Hussein (Simba SC), Nickson Kibabage (Difaa Hassan El-Jadidi - Morocco), David Bryson (Gwambina FC), Bakari Nondo (Coastal Unon), Agrey Morris (Azam FC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Dickon Job (Mtibwa Sugar), Erasto Nyoni (Simba SC), Said Juma ‘Makapu’ (Yanga SC) na Abdi Banda (Highlands Park FC – Afrika Kusini).
    Viungo ni Jonas Mkude (Simba SC), Himid Mao (ENPPI - Misri), Bryson Raphael (Azam FC), Mapinduzi Balama (Yanga SC), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Hassan Dilunga (Simba SC), Feisal Salum (Yanga SC), Lucas Kikoti (Namungo FC), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC), Farid Mussa (CD Tenerife - Hispania) na Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi - Morocco).
    Washambulaji ni; Ayoub Lyanga (Coastal Union), Reliants Lusajo (Namungo FC), Ditram Nchimbi (Yanga SC), John Bocco (Simba SC), Shaaban Iddi Chilunda (Azam FC), Sixtus Sabilo (Polisi Tanzania) na Nahodha Mbwana  Samatta (Aston Villa - England).
    Ndayiragije amesema wachezajj wa Yanga watachelewa kuingia kambini kwa sababu wameruhusiwa kuichezwa klabu yao mechi ya kiporo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Namungo Jumapili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YAFUTA MECHI ZA TAIFA STARS NA TUNISIA KUFUZU AFCON 2021 KWA SABABU YA CORONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top