• HABARI MPYA

    Monday, March 30, 2020

    KAKOLANYA HANA KINYONGO NA AISHI MANULA KUDAKA MECHI NYINGI ZAIDI YAKE SIMBA SC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIPA wa pili wa Simba SC, Benno David Kakolanya amesema kwamba hana kinyongo mwenzake, Aishi Salum Manula akidaka mechi nyingi, kwa sababu wote wapo kwa maslahi ya timu.
    Kakolanya ameyasema hayo wakati akijibu maswali ya mashabiki wa Simba SC kupitia kurasa za Twitter, Facebook na Instagram za klabu jana mchana. 
    “Anapopata mwenzangu ya nafasi ya kucheza (Aishi Manula) ni sawa sawa nimecheza mimi, ni sawa sawa amecheza Ally Salim. Kwa hiyo inakuwa ni sababu ya timu, siyo nafasi ya mtu mmoja mmoja,” alisema Kakolanya.

    Kakolanya yupo katika msimu wake wa kwanza Simba SC tangu asajiliwe kutokana kwa mahasimu wa jadi, Yanga SC Julai mwaka huu.
    Kama ilivyo kwa wachezaji wengine waliosajiliwa kutoka Yanga SC msimu huu, beki wa kushoto Gardiel Michael Mbaga na kiungo Ibrahim Ajibu Migomba – naye ameshindwa kujihakikishia namba kwenye kikosi cha Simba SC.
    Na wakati msimu unaelekea ukingoni, Kakolanya amedaka mechi 23 tu za mashindano yote zikiwemo na za kirafiki Simba SC na kufungwa jumla ya mabao 15. 
    REKODI YA BENNO KAKOLANYA SIMBA SC
    1.  Simba SC 4-0 Orbit Tvet (Aliingia hakufungwa Rusternburg) 
    2. Simba SC 4-1 Platnums Stars (Hakufungwa alimpisha Ali Salim kipindi cha pili Rusternburg)
    3. Simba SC 1-1 Township Rollers (Hakufungwa alimpisha Ali Salim kipindi cha pili Rusternburg)
    4. Simba SC 1-1 Orlando Pirates (Alifungwa moja, alimpisha Ali Salim kipindi cha pili Rusternburg)
    5. Simba SC 3-1 Dynamos (Alifungwa moja, kirafiki Simba Day Taifa)
    6. Simba SC 0-0 UD Songo (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa Beira)
    7. Simba SC 4-2 Azam FC (Alifungwa mbili Ngao ya Jamii Taifa)
    8. Simba SC 1-0 Bandari FC (Hakufungwa kirafiki Taifa)
    9. Simba SC 0-0 Aigle Noir FC (Hakufungwa Kirafiki Kigoma)
    10. Simba SC 1-2 KMC (Alifungwa mbili Kirafiki Chamazi)
    11. Simba SC 1-0 JKT Tanzania (Hakufungwa Kirafiki Chamazi)
    12. Simba SC 6-0 AFC Arusha (Hakufungwa Kombe la TFF Uhuru)
    13. Simba SC 4-0 Lipuli FC (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    14. Simba SC 0-0 (Penalti 3-2) Azam FC (hakufungwa, aliokoa penalti ya Razack Abalora Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan)
    15. Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar  (Alifungwa moja Fainali Kombe la Mapinduzi Amaan)
    16. Simba SC 2-1 Mbao FC  (Alifungwa moja Ligi Kuu Kirumba)
    17. Simba SC 4-1 Alliance FC  (Alifungwa moja Ligi Kuu Kirumba)
    18. Simba SC 2-1 Mwadui FC  (Alifungwa moja Kombe la TFF Taifa)
    19. Simba SC 3-2 Mwadui FC  (Alifungwa mbili Ligi Kuu Taifa)
    20. Simba SC 2-0 Coastal Union  (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    21. Simba SC 2-1 Polisi Tanzania  (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    22. Simba SC 0-1 JKT Tanzania  (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
    23. Simba SC 1-1 (Penalti 3-2) Stand Unted  (Alifungwa moja na penalti mbili Kombe la TFF Shinyanga)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAKOLANYA HANA KINYONGO NA AISHI MANULA KUDAKA MECHI NYINGI ZAIDI YAKE SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top