• HABARI MPYA

    Sunday, March 22, 2020

    KELVIN YONDAN ANAVYOZEEKA NA UTAMU WAKE YANGA NA TAIFA STARS

    Na Gift Macha, DAR ES SALAAM
    BEKI wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani ananifurahisha sana.. Kwa mujibu wa taarifa zake katika mtandao wa Football database anatimiza miaka 36 mwaka huu.. Umri wa soka.. Umri mkubwa sana..
    Ni beki mmoja tu anayecheza kwenye timu kubwa ya VPL ambaye amemzidi umri Yondani.. Unajua ni nani? Ni Aggrey Morris wa Azam FC.. Aggrey amezaliwa miezi saba kabla ya Yondani.. Inafurahisha sana.
    Wapo wengine wakubwa zaidi kama Juma Nyosso wa Kagera Sugar lakini wameshaondoka katika ushindani huu wa juu.. Huu wa kina Aggrey na Yondani
    Kinachonisisimua kuhusu Yondani ni kwamba katika umri wake huo bado ameendelea kuwa GUMZO.. Bado ni tegemeo.. Bado kuondoka au kubaki kwake Yanga kumeendelea kuwa stori kubwa.
    Yawezekana Yondani amejitunza sana.. Amejitahidi sana kulinda kiwango chake.. Siku zote amejitahidi kuishi katika ubora wake na ndiyo sababu anazidi kusumbua. Ni jambo la kumpongeza sana.
    Yondani tangu amejiunga na Simba mwaka 2006 hakuwahi kushuka kiwango.. Aliendelea kuwa bora zaidi alipotua Yanga mwaka 2012.. Miaka yote nane ambayo amekuwa Yanga, ameendelea kuwa chaguo la kwanza.
    Pamoja na kwamba Yondani ameendelea kujipambanua kama beki bora wa kati, nadhani pia Yanga ilichelewa kumtafuta mrithi wake.. Na bahati mbaya mpaka sasa bado wanahaha kumpata mbadala wake.. Ni kama vile Simba ilivyohaha baada ya kuachana na Yondani wakati ule.
    Alipoondoka Canavaro nadhani Yanga ilipaswa kumtafuta na mrithi wa Yondani.. Umri wao haukutofautiana sana.. Ilikuwa wazi.. Bahati mbaya hawakufanya hivyo.. Simba pia kwa sasa inafanya kosa hilo hilo.. Kuendelea kuwategemea Wawa na Nyoni ambao umri umekwenda.. Ni tatizo..
    Hata hivyo bado kama nchi tuna changamoto kubwa ya kuwapata mabeki wa kati wa kizazi kipya.. Angalau kwa sasa yupo Bakari Mwamnyeto.. Erasto Nyoni, Aggrey na Yondani wote wako katika machweo ya soka lao.. Hatuwezi kuwa nao miaka mitatu ijayo katika timu ya Taifa.. Tunahitaji kupata warithi wao..
    Nadhani pamoja na yote, tumpongeze Yondani kuendelea kusumbua katika miaka yake ya mwisho ya soka.. Ni wachache sana waliofanikiwa kama yeye.. Mmojawapo ni Nadir Haroub 'Cannavaro'.. Beki wa Mpira..
    (Gift Macha ni mwandishi wa habari, mtangazaji, mtayarishaji na mchambuzi wa Azam TV unaweza kumfollow instagram @giftmacha_officia ) 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KELVIN YONDAN ANAVYOZEEKA NA UTAMU WAKE YANGA NA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top