• HABARI MPYA

  Saturday, March 14, 2020

  TIMU YA U16 YA TANZANIA YAICHAPA LIBERIA 3-2 KATIKA MCHEZO WA MWISHO WA KIRAFIKI BAINA YAO LEO

  Kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 16 kimeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Liberia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Liberia leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
  Mabao ya Tanzania inayofundishwa na Maalim Saleh 'Romario' yamefungwa na Thabit Thrishan, Hamisi Mohamed na Boniface James. 

  Mechi mbili za awali baina ya timu hizo, Tanzania ilishinda 3-0 Machi 10 kaba ya kufungwa 3-1 Machi 12. Tanzania na Liberia zimelazimika kucheza mara tatu baada ya waalikwa wengine, Malawi kutotokea. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA U16 YA TANZANIA YAICHAPA LIBERIA 3-2 KATIKA MCHEZO WA MWISHO WA KIRAFIKI BAINA YAO LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top