• HABARI MPYA

    Tuesday, March 10, 2020

    SAMATTA MAMBO MAGUMU, ASTON VILLA YACHAKAZWA 4-0 NA LEICESTER CITY KING POWER

    Na Mwandishi Wetu, LEICESTER 
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amecheza kwa dakika zote 90, timu yake, Aston Villa ikiendelea kuvurunda katika Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa 4-0 na wenyej, Leicester City Uwanja wa King Power.
    Kipigo kinazidi kuiporomosha Aston Villa inayofundishwa na kocha Muingereza, Dean Smith sasa ikibaki na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kukamata nafas ya 19, ikiizidi pointi nne Norwich City inayoshika mkia katika ligi ambayo mwisho wa msimu timu tatu zitateremka daraja. 
    Mbwana Ally Samatta aliyejiunga na Aston Villa Januari akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, klabu yake ya kwanza Ulaya iliyomtoa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwaka 2016 ambayo nayo ilimtoa kwao, Tanzania katika klabu ya Simba alikopita akitokea African Lyon – alicheza vizuri na kukarbia kufunga jana.
    Mbwana Samatta alikarbia kufunga jana Aston Villa ikichapwa 4-0 na Leicester City Uwanja wa King Power 

    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Michael Oliver, mabao ya Leicester City inayofundishwa na kocha wa zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers yalifungwa na Harvey Barnes dakika ya 40 na 85 na Jamie Vardy mawili pia, dakika ya 63 kwa penalti na 79.
    Kwa ushindi huo, Leicester City inafikisha pointi 53 baada ya kucheza mechi 29 na kuendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya Manchester City yenye pointi 57 za mechi 28 na Liverpool yenye pointi 82 za mechi 29.
    Kikosi cha Leicester City kilikuwa; Schmeichel, Pereira, Evans, Soyuncu, Justin, Ndidi/Mendy dk84, Albrighton, Praet/Tielemans, Maddison, Barnes na Iheanacho/Vardy dk60. 
    Aston Villa; Reina, Guilbert, Engels, Mings, Targett, Elmohamady/El Ghazi dk64, Douglas, Nakamba, Hourihane/Davis dk67, Grealish na Samatta.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA MAMBO MAGUMU, ASTON VILLA YACHAKAZWA 4-0 NA LEICESTER CITY KING POWER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top