• HABARI MPYA

    Thursday, July 04, 2019

    AZAM FC YAWASAILI SALAMA KIGALI KUWANIA TAJI LA TATU MFULULIZO KOMBE LA KAGAME

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Azam FC kimewasili salama mjini Kigali nchini Rwanda tayari kuanza kutetea taji lake la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame. 
    Mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo, Azam FC wamepangwa Kundi B pamoja na wenyeji, Mukura Victory, KCCA ya Uganda na Bandari ya Kenya.
    Kundi A linaundwa na wenyeji, Rayon Sports, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Atlabara ya Sudan Kusini na KMC ya Dar es Salaam.
    Kundi C linaundwa na wenyeji wengine, APR, Green Eagles ya Zambia, Proline ya Uganda na Heegan ya Somalia wakati Kundi D kuna DC Motema Pembe ya DRC, Gor Mahia ya Kenya, Port ya Djibouti na KMKM ya Zanzibar.
    Kipa Mghana, Razack Abalora (kushoto) na mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma baada ya kiuwasili Kigali
      
    Azam FC wanawania kutwaa taji la tatu mfululizo la Kombe la Kagame katika michuano ya mwaka huu, baada ya awali kulichukua mara mbili mfululizo nyumbani, Tanzania.
    Mwaka 2015 walibeba taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya 2-0 katika fainali Agosti 2 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, mabao ya John Bocco dakika ya 17 na Kipre Herman Tchetche dakika ya 64.
    Wakatetea taji hilo Julai 13 mwaka jana Dar es Salaam baada ya kuifunga Simba SC 2-1, mabao yake yakifungwa na mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda dakika ya 33 na beki Aggrey Moris dakika ya 69, huku la Wekundu wa Msimbazi likifungwa na Kagere Meddie dakika ya 63.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAWASAILI SALAMA KIGALI KUWANIA TAJI LA TATU MFULULIZO KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top