• HABARI MPYA

    Wednesday, July 31, 2019

    HIMID MAO AJIUNGA NA ENPPI BAADA YA PETROJETI KUSHUKA DARAJA LIGI KUU MISRI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami ‘Ninja’ amesaini mkataba wa kujiunga na klabu ya klabu ya ENPPI ya Ligi Kuu ya Misri.
    Mkami anajiunga na ENPPI baada ya klabu yake, Petrojet kushuka Daraja kwenye Ligi Kuu ya Misri baada ya msimu uliopita. 
    “Nina furaha kujiunga na klabu yangu mpya, ENPPI na ninaelekeza nguvu zangu katika msimu mpya kwa ajili ya mafanikio zaidi,”amesema Mao akizungumza baada ya kutambulishwa katika klabu hiyo.

    Himid Mao ‘Ninja’ amejiunga na ENPPI baada ya Petrojet kushuka daraja Misri 

    Mao alijiunga na Petrojet Juni mwaka jana akitokea Azam FC, klabu iliyomuinua kisoka nchini Tanzania akianza kuichezea ngazi ya timu za vijana.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyerithi kipaji cha baba, Mao Mkami ‘Ball Dancer’, kiungo wa zamani wa Pamba, Mtibwa Sugar na Moro United aliibukia akademi ya Elite mwaka 2005 kabla ya 2007 kujiunga na Azam.
    Mao ni mchezaji aliyeanza kuchezea timu za vijana za taifa Tanzania kuanzia umri chini ya miaka 15, U17, U20, U23 na hadi sasa ya wakubwa na tangu mwaka 2013 ameichezea Taifa Stars mechi 50 na kuifungia mabao mawili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HIMID MAO AJIUNGA NA ENPPI BAADA YA PETROJETI KUSHUKA DARAJA LIGI KUU MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top