• HABARI MPYA

    Thursday, July 04, 2019

    KAGERA SUGAR YASAJILI WAWILI WA MBEYA CITY NA MMOJA WA MBAO FC KUIMAIRSHA KIKOSI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BAADA ya kunusurika kushuka daraja, Kagera Sugar ya Bukoba imejiimarisha kwa kusajili wachezaji wapya watatu kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
    Hao ni beki Erick Kyaruzi ‘Mopa’ na washambuliaji Frank Ikobela, wote kutoka Mbeya City ya Mbeya na  Evarist Mjwahuki kutoka Mbao FC ya Mwanza.
    Taarifa ya Kagera Sugar imesema; “Erick Kyaruzi karudi nyumbani akitokea Mbeya City, beki kisiki. Washambuliaji Frank Ikobela na  Evarist Mjwahuki nao wamejiunga na timu yetu,”.
    Kagera Sugar na Mwadui FC zilinusurika kushuka daraja baada ya kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kupitia mechi zao Play-Off dhidi ya Pamba SC na Geita Gold Mine za Daraja la Kwanza.
    Mshambuliaji chipukizi, Frank Ikobela akisaini mkataba wa kujiunga na Kagera Sugar kutoka Mbeya City

    Mabao ya Ally Ramadhani dakika ya 51 na Japhet Makalayi dakika ya 59 yaliipa Kagera Sugar ushindi wa 2-0 dhidi ya Pamba SC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Juni 9 baada ya timu hizo kutoka sare ya kwenye mchezo wa kwanza Juni 3 Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
    Na hiyo ni baada ya Kagera Sugar kumaliza nafasi ya 18 katika Ligi Kuu, nyuma ya Mwadui FC iliyomaliza nafasi ya 17 ambayo iliitoa Geita Gold katika mechi ya mchujo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR YASAJILI WAWILI WA MBEYA CITY NA MMOJA WA MBAO FC KUIMAIRSHA KIKOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top