• HABARI MPYA

  Thursday, July 04, 2019

  KIUNGO WA HARAMBEE STARS, FRANCIS KAHATA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI SIMBA SC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Kenya, Francis Kahata Nyambura amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba SC akitokea Gor Mahia ya kwao.
  Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba klabu imevutiwa na Kahata baada ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Kenya akiwa na Gor Mahia kabla ya kwenda kung’ara kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwezi huu nchini Misri.
  “Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza eneo la kiungo, kwasasa akiwa sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya kinachoshiriki Afcon, Francis Kahata (27) msimu ujao atavaa jezi ya Mabingwa wa nchi baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili,”imesema taarifa yua Simba na kuongeza;
  “Akiwa kwenye klabu hiyo (Gor Mahia) alishinda Kombe la Ligi Kuu mara tatu, kiungo bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Kenya mara mbili na mchezaji bora wa msimu 2018/2019 wa Gor Mahia,”.
  Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Crescentius Magori (kushoto) akimtambulisha Francis Kahata baada ya kusaini mkataba leo  

  Kahata anakuwa mchezaji mpya wa tisa kusajiliwa Simba SC na wa sita wa kigeni baada ya Wabrazil mabeki beki Gerson Fraga Vieira ATK ya Ligi Kuu ya India na Tairone Santos da Silva kutoka klabu ya Atletico Cearense FC, mshambuliaji, Wilker Henrique da Silva kutoka Bragantino, zote za Daraja la Nne nchini Brazil na viungo Msudan Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman na winga Deo Kanda kutoka TP Mazembe ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Wengine watatu ni wazawa, kipa Beno Kakolanya, kiungo Ibrahim Ajibu kutoka Yanga SC ya Dar es Salaam na beki Kennedy Wilson Juma kutoka Singida United ya Singida.
  Pamoja na kusaini wachezaji wapya, Simba SC pia imewapa mikataba mipya wachezaji wake kadhaa wa msimu uliopita, wakiwemo kipa Aishi Manula, mabeki Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Nahodha Msaidizi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala, Muivory Coast, Serge Wawa Pascal viungo Jonas Mkude, Mzambia Clatous Chama na washambuliaji Nahodha Mkuu, John Bocco na Meddie Kagere raia wa Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIUNGO WA HARAMBEE STARS, FRANCIS KAHATA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top