• HABARI MPYA

    Monday, July 15, 2019

    NGASSA APIGA ‘HAT TRICK’ YANGA SC YASHINDA 10-1 MECHI YA KIRAFIKI MOROGORO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Yanga SC leo imetoa onyo baada ya kushinda mabao 10-1 dhidi ya wenyeji, Tanzanite katika mchezo wa kirafiki wa mazoezi uwanja wa Chuo cha Biblia, Bingwa mkoani Morogoro ambako imeweka kambi kujiandaa na msimu mpya. 
    Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa aliyefunga mabao matatu peke yake dhidi ya timu hiyo ya vijana chini ya umri wa miaka 20.
    Mabao mengine yamefungwa na Feisal Salum, Raphael Daudi, Mapinduzi Balama, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi, Wanyarwanda Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Mganda Juma Balinya, 
    Wakati huo huo: mshambuliaji mpya wa Yanga, Sadney Urikhob amewasili nchini jana na leo anatarajia kuungana na wachezaji wenzake Morogoro.

    Mrisho Ngassa (kulia) akikabidhiwa mpira baada ya kufunga hat-trick leo Morogoro

    Urikhob amechelewa kujiunga mapema kambini kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo hakuweza kujiunga kikosini kwa muda mwafaka.
    Yanga itamenyana na vigogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), AS Vita katika mchezo wa kirafiki Agosti 4, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Mchezo huo utafanyika katika kilele cha Wiki Mwanachi, tamasha maalum la kutambulisha kikosi kipya cha klabu pamoja na jezi za msimu.
    Kwa sasa kikosi cha Yanga SC kipo kambini mjini Morogoro chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Msambia Noel Mwandila kikijiandaa na msimu mpya na Kocha Mkuu, Mkongo Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwa amewasili hadi mapema wiki ijayo. 
    Wachezaji wanaotarajiwa kuchezea Yanga msimu ujao ni makipa; Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili na Klaus Kindoki. 
    Mabeki; Paul Godfrey ‘Boxer’, Juma Abdul, Muharami Issa ‘Marcelo’, Jaffary Mohamed, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Ally Ally, Mustafa Suleiman, Ally Mtoni ‘Sonso’ na Lamine Moro.
    Viungo; Papy Kabamba Tshishimbi, Said Juma ‘Makapu’, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Mohamed Issa ‘Banka’, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Mapinduzi Balama, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Raphael Daud Loth na Abdulaziz Makame ‘Bui’.
    Washambuliaji; Sadney Khoetage, Juma Balinya na Kalengo Maybin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA APIGA ‘HAT TRICK’ YANGA SC YASHINDA 10-1 MECHI YA KIRAFIKI MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top