• HABARI MPYA

  Thursday, October 18, 2018

  MTIBWA SUGAR YAMTIA PINGU MSHAMBULIAJI WAKE CHIPUKIZI RIPHAT KHAMIS HADI 2021

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa Mtibwa Sugar, Riphat Khamis amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
  Manejimenti ya timu ya Mtibwa imekuwa na utaratibu wa kuimarisha mikataba ya wachezaji kabla ya mikataba yao kufika tamati, mkataba wa Riphat Khamis na Mtibwa ulikuwa unafika tamati mwishoni mwa msimu huu na pande zote mbili zimefikia muafaka wa kuboresha mkataba wa awali.
  Hivyo mkataba huu ulioboreshwa wa mshambuliaji kinda wa timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes Riphat Khamis na Mtibwa Sugar utafika tamati 2021.

  Riphat Khamis aliumia enka katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa ligi kuu bara na kumfanya kuitumikia Mtibwa katika michezo mitatu pekee hadi sasa katika msimu huu, katika michezo hiyo mitatu Riphat Khamis amefanikiwa kutoa pasi za magoli (assist) mbili.
  Riphat aliumia katika mchezo namba 25 wa ligi kuu bara dhidi ya Mbeya City uliochezwa tarehe 1.09.2018 katika dimba la Manungu, Jeraha hilo la enka lilimuweka nje mshambuliaji huyo kwa siku 40 na tayari ameanza mazoezi mepesi ili kujiweka sawa.
  Msimamizi wa masuala ya sheria wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabr amesema kwamba taratibu zote zimefuatwa katika kusiani mkataba huo.
  “Ni kweli tumeingia kandarasi mpya ya miaka miwili na Riphat na tunataraji makubwa kutoka kwake kutokana na kipaji kikubwa alicho nacho, walimu walitueleza mipango yao juu yake hivyo tuliamua kuingia kandarasi mpya na Riphat” Abubakar Swabr.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAMTIA PINGU MSHAMBULIAJI WAKE CHIPUKIZI RIPHAT KHAMIS HADI 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top