• HABARI MPYA

  Tuesday, October 02, 2018

  KAGERA SUGAR NA KMC, ALLIANCE NA NDANDA FC WOTE 0-0, TFF YASEMA LIGI HAISIMAMI TENA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  MECHI zote za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zilizofanyika leo zimemalizika kwa sare ya bila kufungana baina ya Alliance FC na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza na Kagera Sugar dhidi ya KMC ya Kinondoni Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Matokeo hayo yanaiongezea kila timu pointi moja, Kagera Sugar inafikisha 11 katika mechi ya saba, KMC na Ndanda FC pointi pointi nane katika mechi ya nane na Alliance FC pointi tano katika mechi ya nane.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu unafuatia hivi sasa kati ya wenyeji, Azam FC dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

  Wachezaji wa Alliance FC na Ndanda FC leo Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza

  Wakati huo huo: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kwamba mechi za Ligi Kuu hazitaahirishwa kupisha kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa na michezo miwili ya nyumbani na ugenini dhidi ya Capoe Verde Oktoba 12 mjini Praia na Oktoba 16 Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR NA KMC, ALLIANCE NA NDANDA FC WOTE 0-0, TFF YASEMA LIGI HAISIMAMI TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top