• HABARI MPYA

  Wednesday, October 03, 2018

  AL AHLY YATANGULIZA MGUU MMOJA FAINALI LIGI YA MABINGWA

  TIMU ya Al Ahly imetanguliza mguu mmoja Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Entente Setif ya Algeria katika Nusu Fainali ya kwanza Uwanja wa jeshi wa Al Salam mjini Cairo, Misri.
  Kiungo mkongwe, Walid Soliman alianza kuifungia Al Ahly dakika ya 23 kabla ya Islam Mohareb kufunga la pili dakika tatu kabla ya mapumziko.
  Ushindi huo unaifanya Al Ahly ifikishe mechi saba za kucheza bila kufungwa kwa mabingwa hao wa rekodi wa Ligi ya Mabingwa, mara nane tangu kocha Mfaransa, Patrice Carteron aanze kazi mwaka huu.


  Islam Mohareb (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kuifungia bao la pili Al Ahly jana

  Kilikuwa kipigo cha kwanza katika mechi saba za michuano ya Afrika kwa washindi mara mbili, Setif, ambao waliwatoa mabingwa watetezi Wydad Casablanca ya Morocco katika Robo Fainali.
  Ahly ingevuna ushindi mnono kama si mabao ya Mmorocco Walid Azaro na mzawa Ahmed Hamoudi kukataliwa kwa sababu walikuwa wamezidi.
  Mashabiki wenye mapenzi makubwa na timu yao, wa Ahly watasafiri kwenda kuisapoti katika mchezo wa marudiano nchini Algeria Oktoba 23. 
  Ahly pia iliifunga Setif 2-0 nyumbani kwake walipokutana mara ya mwisho kwenye Nusu Fainali miaka 30 iliyopita, lakini Wamisri hao wakatolewa kwa penalti baada ya sare ya jumla.

  Kiungo wa Esperance, Ayman Ben Mohamed akipasua katikati ya wachezaji wa Primiero de Agosto

  Mapema katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali uliotangulia jana, Primeiro de Agosto ya Angola iliifunga Esperance ya Tunisia 1-0 mjini Luanda, bao la dakika ya 80 la Luvumbo 'Bua' Pedro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY YATANGULIZA MGUU MMOJA FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top