• HABARI MPYA

  Sunday, January 22, 2017

  SIMBA SC YAWALIPUA MAAFANDE 2-0 NA KWENDA 16 BORA KOMBE LA TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imeifuata Yanga hatua ya 16 Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Dar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo.
  Ahsante kwa wafungaji wa mabao hayo, mshambuliaji Pastory Athanas kipindi cha kwanza na beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kipindi cha pili. 
  Dar es Salaam. Ni mpira wa ovyo uliochosha macho ya watazamaji wachache waliojitokeza kwenye uwanja wa Uhuru jana licha ya wengi kutegemea kuwa Simba ingemaliza kipindi cha kwanza ikiwa na mabao mengi dhidi ya Polisi Dar.
  Mohammed Hussein 'Tshabalala' (kushoto) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la pili 

  Pastory Athanas akikimbi kushangilia baada ya kufunga bao la kwanza
  Pastory Athanas (kulia) akimtoka beki wa Polisi
  Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib akimtoka beki wa Polisi


  Simba ilipata bao lake la kwanza mapema la dakika ya tatu, Pastory Athanas akiunganisha pasi ya Shiza Kichuya ambaye awali alipokea mpira mrefu wa kiungo na Nahodha Jonas Mkude.
  Zaidi ya bao hilo, timu zote mbili zilishindwa kuonyesha mipango na soka la kuvutia licha kukosa nafasi kadhaa ambazo hazikuonekana kupatikana kutokana na ustadi wa kutengenezwa kipindi cha kwanza.
  Polisi Dar wataijutia nafasi waliyoipata dakika ya 13 ambapo Paschal Theodory akiwa yeye na kipa Daniel Agyei alishindwa kuipatia timu yake bao la kusawazisha baada ya kumbabatiza kipa huyo wa Simba.
  Simba walijibu shambulizi hilo dakika ya 16 na 18 kupitia mashuti ya Athanas na Muzamiru Yassin lakini yote yaliishia mikononi mwa kipa wa Polisi Dar, Kondo Salum.
  Kipindi cha pili Polisi Dar walirudi kwa nguvu na kuongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Simba na kuufanya mchezo uzidi kuwa mzuri.
  Hata hivyo, nyota ya Simba iliendelea kung’ara kwa kutengeneza nafasi nzuri zaidi za kufunga ambazo washambuliaji wake walsihindwa kuzitumia vizuri.
  Hatimaye beki Tshabalala akawasaidia kazi washambuliaji wa Simba SC kwa kufunga bao la zuri la pili dakika ya 82 kwa kichwa baada ya mpira wa juu wa Said Ndemla.  
  Henerico nusura aipatie bao Polisi Dar dakika ya 76 kama si kipa wa Simba, DanielAgyei kudaka shuti lake.
  Mechi nyingine za leo Kombe la TFF Ruvu Shooting imetolewa na Kiluvya FC kwa kufungwa 2-1, Tanzania Prisons imeitoa Mbeya Kwanza kwa mabao 2-1 na Toto Africans imeitoa Mwadui FC kwa penalti 5-4 baada ya sare 2-2.
  Kikosi cha Simba kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Method Mwanjali, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Ibrahim Hajib/Said Ndemla dk58, Pastory Athanas/Laudit Mavugo dk66 na Mwinyi Kazimoto/Jamal Mnyate dk58.
  Polisi Dar; Kondo Salum, Musiba Suleiman, Abbas Kapombe, Thabit Amnyishe, Godfrey Mpewembwe, Vincent Thedeo, Evance Wilfred/Paul Makula dk78, Henerico Sylavanus, Paschal Theodor, Hamad Kambangwa/Toto Stanslaus dk88 na Nassor Habib/Mateso Baraka dk74.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWALIPUA MAAFANDE 2-0 NA KWENDA 16 BORA KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top