• HABARI MPYA

  Sunday, January 22, 2017

  MWANJALI MCHEZAJI BORA LIGI KUU DESEMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa Simba, Method Mwanjali amechaguliwa kuwa mchezaji bora Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017. 
  Beki huyo wa kati, aliwashinda kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima na beki Yakubu Mohamed wa Azam FC. Mwezi Desemba ulichezwa raundi tatu za Ligi hiyo, huku Simba ikicheza mechi mbili ugenini na moja nyumbani. Raundi hizo ni ya 16, 17 na 18.
  Mwanjali (kushoto) akiiichezea SImba SC dhidi ya African Lyon

  Mwanjali aliiongoza Simba kushinda mechi zote tatu, hivyo timu yake kupata ushindi wa asilimia 100 kwa kunyakua pointi zote tisa, na kubaki katika nafasi yao ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi, nafasi ambayo walikuwa nayo wakati wanaingia raundi ya 16.
  Pia katika raundi hizo tatu ambapo Simba haikufungwa bao hata moja, Mwanjali alicheza dakika zote 270, na bila kuonyeshwa kadi yoyote. Alichangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya timu yake huku akiongoza safu ya ulinzi.
  Kwa kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora, Mwanjali atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wakuu wa Ligi hiyo Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
  Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mchezaji bora kwa msimu wa 2016/2017 hadi sasa ni John Raphael Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Ramadhan Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Happygod Msuva wa Yanga (Oktoba), na Rifati Hamisi wa Ndanda (Novemba).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWANJALI MCHEZAJI BORA LIGI KUU DESEMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top