• HABARI MPYA

  Sunday, January 22, 2017

  ARSENAL PUNGUFU YAITWANGA BURNLEY 2-1 EMIRATES

  Shkodran Mustafi akiruka kichwa katikati ya wachezaji wa Burnley kuifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 59 katika ushindi wa 2-1 leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates. Bao la pili la Arsenal lilifungwa na Alexis Sanchez kwa penalti dakika ya nane ya muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida kufuatia ya Laurent Koscielny kuchezewa rafu, wakati la Burnley lilifungwa na Andre Gray dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya dakika 90. Granit Xhaka alitolewa kwa kadi nyekundu kwa mara ya pili msimu huu na mara ya tisa ndani ya miaka mitatu baada ya kumuingia kwa miguu yote miwili kiungo wa Burnley, Steven Defour dakika ya 65 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL PUNGUFU YAITWANGA BURNLEY 2-1 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top