• HABARI MPYA

    Tuesday, February 09, 2016

    YANGA SC YABEBA ‘JESHI LA MAANGAMIZI’ SAFARI YA MAURITIUS, KAMUSOKO NA CANNAVARO WOTE NDANI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA SC inatarajiwa kuondoka na kikosi chake kamili kesho kwenda Mauritius kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Cercle de Joachim. 
    Hata hivyo, Yanga SC haijajua itaondoka na ndege ya saa ngapi kwa sababu Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SA) limeshindwa kuwapatia ndege ya kuunganisha mapema mjini Johannesburg, kwenda Curepipe, Mauritius.  
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba kwa sasa uongozi unawasiliana na Shirika la Ndege la Afrika Kusini ili kujua ratiba kamili ya safari.
    “Ndege ya mapema ambayo tulitarajia kuunganisha Johannesburg kwenda Mauritius bahati mbaya imejaa, sasa SA wanatutafutia ndege nyingine, maana yake hatujajua na hapa watatupangia ndege ya saa ngapi tuondoke nayo,”amesema Muro.
    Lakini Muro amesema kila kitu kipo sawa, isipokuwa ni SA wenyewe na ratiba zao za ndege za kuunganisha kuanzia Johannesburg ndiyo inawafanya hadi sasa wawe hawajajua ratiba yao kamili ya safari.
    Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi kuanzia Saa 9:30 Alasiri kwa saa za Mauritius Uwanja wa Curepipe mjini Curepipe na Pluijm amebebea karibu kikosi chake chote, akiacha wachezaji watatu tu.
    Hao ni kipa wa tatu, Benedicto Tinocco, kiungo Godfrey Mwashiuya na mshambuliaji Matheo Anthony. 
    Wachezaji waliokuwa majeruhi, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Amissi Tambwe wote watasafiri na timu.
    Mkuu wa Msafara ni Ayoub Nyenzi, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakati upande wa viongozi wanakwenda Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit na Muro.

    KIKOSI KINACHOKWENDA MAURITUS;
    Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.
    Mabeki; Juma Abdul, Mbuyu Twite (DRC), Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Vincent Bossou (Togo) na Pato Ngonyani.
    Viungo ni; Said Juma ‘Makapu’, Salum Telela, Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Haruna Niyonzima (Rwanda), Simon Msuva, Issoufou Boubacar (Niger) na Deus Kaseke.
    Washambuliaji ni; Malimi Busungu, Paul Nonga, Amissi Tambwe (Burundi) na Donald Ngoma (Zimbabwe).
    Kocha Mkuu wa Yanga SC, Hans van der Pluijm kushoto amebeba karibu kikosi chake chote kwa safari ya Mauritius

    BENCHI LA UFUNDI; 
    Kocha Mkuu; Hans van der Pluijm (Uholanzi)
    Kocha Msaidizi; Juma Mwambusi
    Kocha wa Makipa; Juma Pondamali
    Daktari; Nassor Matuzya
    Meneja; Hafidh Saleh
    Mchua Misuli; Jacob Onyango
    Mtunza Vifaa; Mohammed Mpogolo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YABEBA ‘JESHI LA MAANGAMIZI’ SAFARI YA MAURITIUS, KAMUSOKO NA CANNAVARO WOTE NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top