• HABARI MPYA

  Sunday, February 14, 2016

  SPURS YAIKALISHA MAN CITY ETIHAD, LIVERPOOL YAIKUNG'UTA ASTON VILLA 6-0 VILLA PARK

  Kiungo Mdenmark wa Tottenham, Christian Eriksen (kulia) akiruka 'kwanja' la beki wa Manchester City, Vincent Kompany katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad mjini Manchester. Spurs ilishinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Harry Kane kwa penalti dakika ya 53 baada ya Raheem Sterling kuunawa mpira kwenye boksi na Eriksen dakika ya 83, wakati la City limefungwa na Mnigeria, Kelechi Iheanacho PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mshambuliaji Mbelgiji wa Liverpool, Divock Origi akifumua shuti pembeni ya beki wa Aston Villa, Jores Okore kuifungia timu yake katika ushindi wa 6-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Villa Park. Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Daniel Sturridge, James Milner, Emre Can, Nathaniel Clyne na Kolo Toure PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SPURS YAIKALISHA MAN CITY ETIHAD, LIVERPOOL YAIKUNG'UTA ASTON VILLA 6-0 VILLA PARK Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top