• HABARI MPYA

  Sunday, February 14, 2016

  HUGO BROOS NDIYE KOCHA WA 'SIMBA WASIOFUNGIKA' WA CAMEROON

  MBELGIJI Hugo Broos (pichani kushoto) ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Cameroon leo, hii ikiwa na kazi yake ya kwanza kufundisha mwaka huu.
  Shirikisho la Soka Cameroon (FECAFOOT), limetangaza rasmi leo mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 63 kupitia tovuti yake.
  Beki huyo wa zamani wa kimataifa, Broos alijipatia umaarufu kama kocha wakati alipokuwa akiiongoza Club Brugge ya nyumbani kwao, hadi ikatwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya Ubelgiji mwaka 1992 na mwaka 1996, kabla ya kutwaa pia taji la Daraja la Kwanza alipokuwa akiifundisha Anderlecht mwaka 2004.
  Mara ya mwisho kabisa aliifundisha kwa miezi mitano NA Hussein Dey ya Algeria.
  Simba Wasiofungika wamekjuwa chini ya kocha wa muda, Alexandre Belinga tangu kuondoka kwa Mjerumani, Volker Finke na sasa atakuwa mmoja wa wasaidizi wawili wa Broos, pamoja na Mbelgiji mwenzake mwenye umri wa miaka 36, Sven VandenBroeck.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HUGO BROOS NDIYE KOCHA WA 'SIMBA WASIOFUNGIKA' WA CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top