• HABARI MPYA

  Wednesday, February 10, 2016

  SERENGETI BOYS YAPEWA SHELISHELI KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA 2017 MADAGASCAR

  TANZANIA imepangwa kuanza na Shelisheli katika michuano ya kufuzu Fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zitakazofanyika nchini Madagascar mwakani.
  Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba mechi mbili zitachezwa Juni mwaka huu, nyumbani na ugenini baina ya Serengeti Boys na Shelisheli na mshindi wa jumla atakutana na Afrika Kusini katika Raundi ya Pili ya mchujo.

  Mechi ya kwanza inatarajiwa kufanyika kati ya Juni 24,25 na 26 Dar es Salaam, wakati mchezo wa marudaino utachezwa Julai 1, 2 na 3 nchini Shelisheli.
  Kihistoria Tanzania na Shelisheli zimewahi kukutana mara moja katika mechi ya timu za wakubwa mchezo wa kirafiki na zikatoka sare ya 1-1 Juni 9, mwaka 1988.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAPEWA SHELISHELI KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA 2017 MADAGASCAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top