• HABARI MPYA

  Sunday, February 14, 2016

  SAMATTA ATOKEA BENCHI TENA KRC GENK YAUA 6-1 LIGI KUU UBELGIJI

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta (pichani kushoto) ametokea benchi kipindi cha pili na kuisaidia timu yake, KRC Genk kushinda mabao 6-1 dhidi ya Waasland-Beveren katika mchezo wa Ligi Kuu ua Ubelgiji, maarufu kama Pro League usiku huu Uwanja wa Cristal Arena mjini Genk.
  Samatta aliyejiunga na timu hiyo mwezi uliopita kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), aliingia dakika ya 73 kumpokea Nikolaos Karelis, wakati huo tayari Genk 5-1.
  Samatta alikuwa uwanjani tayari, wakati Christian Kabasele anaifungia Genk bao la sita dakika ya 84. Mabao mengine ya Genk yamefungwa na Karelis dakika ya tisa na 31, Neeskens Kebano dakika ya 26, Leon Bailey dakika ya 27 na Thomas Buffel dakika ya72, wakati bao pekee la Waasland-Beveren limefungwa na Zinho Gano dakika ya 18.
  Huo ulikuwa mchezo wa pili mfululizo, Samatta anaingia akitokea benchi tangu asajiliwe na KRC Genk Januari mwaka huu, baada ya Jumamosi iliyopita pia kuingia dakika ya 73 pia kumpokea huyo huyo, Karelis timu hiyo ikishinda 1-0 dhidi ya Mouscron-Peruwelz Uwanja wa Canonnier, bao pekee Buffel dakika ya 63.
  Genk inatarajiwa kushuka tena dimbani Jumamosi ijayo kumenyana na wenyeji, Lokeren Uwanja wa Daknamstadion katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI TENA KRC GENK YAUA 6-1 LIGI KUU UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top