• HABARI MPYA

    Monday, July 14, 2014

    MBUZI WA KAFARA WA BRAZIL ASTAAFU MWAKA MMOJA TANGU AWE SHUJAA WA TAIFA

    MKONGWE Fred amejiuzulu kuichezea Brazil baada ya kufanya vibaya kwenye Kombe la Dunia.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye ameichezea mechi 39 nchi yake, aligeuka mbuzi wa kafara mbele ya mashabiki wa Brazil waliokuwa wakimkandia na kumzomea katika mashindano ya mwaka huu.
    Simanzi: Fred alifanywa mbuzi wa kafara na mashabiki wa Brazil baada ya timu hiyo kuboronga katika Kombe la Dunia

    Fred alizomewa mob wakati Brazil ikitandikwa mabao 7-1 na Ujerumani katika Nusu Fainali mjini Belo Horizonte.
    Hali hii ilijitokeza kiasi cha mwaka mmoja, tangu mshambuliaji huyo wa Fluminense ape we tuzo ya Miatu cha Fedha kwa kuwa mfungaji bora wa Kombe la Mabara, ambalo Brazil walilitwaa wakiwa wenyeji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBUZI WA KAFARA WA BRAZIL ASTAAFU MWAKA MMOJA TANGU AWE SHUJAA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top