MSHAMBULIAJI Alexis Sanchez - ambaye Arsenal wanaamini atawapa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 30 kutka Barcelona.
Nyota huyo wa Chile, ambaye alikatisha mapumziko yake mafupi kwenda kukamilisha uhamisho wake kutua London, amekamilisha vipimo vya afya na kusaini Mkataba wa miaka minne, wenye kipengele cha uwezekano wa kuongezewa miezi 12 ambao utamfanya alipwe mshahara wa Pauni 140,000 kwa wiki.
Kiwango hicho kitamfanya alingane na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani, kiungo Mesut Ozil aliyekuwa anaongoza kulipwa Gunners.
"Nina furaha mno kujiunga na Arsenal, klabu ambayo ina kocha babu kubwa, kikosi chenye wachezaji wazuri haswa, sapoti kubwa dunia nzima na Uwanja mkubwa mjini London,'amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.


Sanchez amesaini Mkataba wa miaka mitano ambao utamfanya alipwe Pauni 140,000 kwa wiki Uwanja wa Emirates



.png)
0 comments:
Post a Comment