IJUMAA ilikuwa siku nzuri kwa Arsenal, ikipata mchezaji mpya, Alexis Sanchez, na zaidi mchumba wa mchezaji huyo Laia Grassi ameingia kwenye orodha ya Wake na Wapenzi wa Wachezaji (WAG) wapenzi wa timu hiyo.
Mspanyola Grassi amedhihirisha mapenzi yake kwa The Gunners baada ya kuposti picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na jezi ya Arsenal.
Wapenzi: Mchezaji mpya wa Arsenal, Sanchez akiwa na mpenzi wake Grassi pichani
Ameandika: "Mimi ni Gunner, kwa Arsene Wenger kutoa Pauni Milioni 30 kumnunua nyota wa Chile kutoka Barcelona.
Sanchez atakuwa anahudhuria la kujifunza Kiingerea kwa wiki mjini London, kabla ya kuanza maisha ya mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hawezi kuzungumza Kiingereza.



.png)
0 comments:
Post a Comment