Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM
MECKY Mexime, kocha wa Mtibwa Sugar, amesema klabu yao haiyumbishwi na klabu kongwe nchini Simba na Yanga kununua nyota wake kwa kuwa inajua mahala pa kupata wachezaji wazuri.
Wiki iliyopita, uongozi wa Simba ulithibisha kumnasa na kumsainisha mkataba wa miaka miwili kipa bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL) msimu huu Hussein Sharrif kutoka Mtibwa Sugar.
Hata hivyo, Mexime ameiambia BIN ZUBEIRY kuwa hana wasiwasi juu ya kuondoka kwa kipa huyo kwa kuwa klabu yao inajua namna ya kuziba pengo lake.
“Tumeshazoea sisi (Mtibwa), si mara ya kwanza Simba na Yanga kuja kuchukua nyota wetu lakini tunarekebisha. Tutaziba mapengo yote kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa ligi kuu,” amesema Mexime.
Nahodha huyo wa zamani wa Mtibwa na timu ya taifa (Taifa Stars), alisema kuna idadi kubwa ya nyota wa Mtibwa waliokchukjuliwa na timu za VPL lakini klabu hiyo itapandisha wachezaji wa kikosi chake cha pili na kusajili baadhi ya wachezaji wazoefu kutoka timu nyingine.
“Kwa sababu ratiba ya ligi imesogezwa, tunaamini hata muda wa usajili utaongezwa na tutakuwa na muda mzuri zaidi wa kuziba mapengo yaliyopo,” amesema zaidi Mexime.
Mbali na Sharif, Mtibwa Sugar inayoongioza kwa kupika wachezaji nyota nchini, imewapoteza pia Juma Mpakala, Salvatory Ntebe na Yusuph Nguya waliotua kwa ‘maafande wa Pwani’, klabu ya Ruvu Shooting.
Katika miaka ya karibuni, kjlabu za Simba na Yanga zimekuwa zikichukua wachezaji wengi nyota kutoka Mtibwa. Baadhi yao ni kipa Shaaban Kado, aliyetua Yanga kwa dau Sh. milioni 50 lakini baadaye akauzwa kwa hasara kwa klabu ya mabingwa wa Tanzania Bara 1988, Coastal Union na washambuliaji Said Bahanunzi na Hussein Javu waliotua Yanga kwa ofa nono pia.

![]() |
| Cassilas kulia akiwa na kiongozi wa Simba SX, Said Tuliy baada kusaini mkataba wa miaka miwili wiki hii |
“Tumeshazoea sisi (Mtibwa), si mara ya kwanza Simba na Yanga kuja kuchukua nyota wetu lakini tunarekebisha. Tutaziba mapengo yote kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa ligi kuu,” amesema Mexime.
![]() |
| Cassilas akimkatalia Jerry Tegete wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu mwaka 2012, akiwa Mtibwa Sugar |
Nahodha huyo wa zamani wa Mtibwa na timu ya taifa (Taifa Stars), alisema kuna idadi kubwa ya nyota wa Mtibwa waliokchukjuliwa na timu za VPL lakini klabu hiyo itapandisha wachezaji wa kikosi chake cha pili na kusajili baadhi ya wachezaji wazoefu kutoka timu nyingine.
“Kwa sababu ratiba ya ligi imesogezwa, tunaamini hata muda wa usajili utaongezwa na tutakuwa na muda mzuri zaidi wa kuziba mapengo yaliyopo,” amesema zaidi Mexime.
Mbali na Sharif, Mtibwa Sugar inayoongioza kwa kupika wachezaji nyota nchini, imewapoteza pia Juma Mpakala, Salvatory Ntebe na Yusuph Nguya waliotua kwa ‘maafande wa Pwani’, klabu ya Ruvu Shooting.
Katika miaka ya karibuni, kjlabu za Simba na Yanga zimekuwa zikichukua wachezaji wengi nyota kutoka Mtibwa. Baadhi yao ni kipa Shaaban Kado, aliyetua Yanga kwa dau Sh. milioni 50 lakini baadaye akauzwa kwa hasara kwa klabu ya mabingwa wa Tanzania Bara 1988, Coastal Union na washambuliaji Said Bahanunzi na Hussein Javu waliotua Yanga kwa ofa nono pia.

.png)
0 comments:
Post a Comment