• HABARI MPYA

  Thursday, July 03, 2014

  ALIYECHEZA KOMBE LA DUNIA ATUA AZAM FC, NI ALIYEFUNGA BAO LA ‘AJABU’ OLIMPIKI 2008 BEIJING

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Haiti, aliyecheza Kombe la Mabara mwaka ya Dunia la FIFA jana nchini Brazil, Leonel Saint-Preux ametua Azam FC kwa ajili ya kujiunga nayo kwa msimu ujao.
  Kocha Joseph Marius Omog raia wa Cameroon amesema amekuwa na mchezaji huyo kwa siku mbili na atahitaji muda zaidi kumuona kabla ya kuamua kumsajili au la.
  Mshambuliaji huyo aliyezaliwa Machi 12, mwaka 1985 in Cap-Haitien mara ya mwisho alichezea klabu ya FELDA United F.C. ya Ligi Kuu ya Malaysia.
  Mshambuliaji wa Haiti ametua Azam FC, je atasajiliwa?
  Hapa anacheza Kombe la Mabara dhidi ya Hispania 

  Kisoka, Saint-Preux alianzia Zenith ya kwao, ambako alikuwa mkali wa mabao katika Ligia ya nchini humo.
  Saint-Preux alisaini Minnesota Thunder ya Daraja la Kwanza Marekani Aprili 15, mwaka 2009, kabla ya kuhamia Hanoi ya Vietnam.
  Machi 2010 alisiani mkataba wa awali na Aztex, lakini akatemwa baada ya kueli vipimo vya afya.
  Kimataifa Saint-Preux, alianzia kuchezea timu za vijana za Haiti wa umri tofauti. Alikuwemo kwenye kikosi cha Haiti kilichofuzu michezo ya Olimpiki mwaka 2008 mjini Beijing, akifunga bao la kukumbukwa kutoka umbali wa mita 40 timu yake ikishinda 2-1 dhidi ya Canada. 
  Alianza kuchezea timu ya wakubwa ya Hati mwaka 2007. Alifunga bao lake la kwanza timu ya taifa ya Haiti Novemba 19, mwaka 2008 katika sare ya 1-1 Surinam. Haiti ilifungwa 10-0 na Hispania kwenye michuano hiyo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALIYECHEZA KOMBE LA DUNIA ATUA AZAM FC, NI ALIYEFUNGA BAO LA ‘AJABU’ OLIMPIKI 2008 BEIJING Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top