• HABARI MPYA

    Thursday, July 03, 2014

    AVEVA AMTEUA DEWJI KUMSAIDIA KAZI HANS POPPE, AUNDA KAMATI ‘NZITO’ YA MASHINDANO

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    RAIS mpya wa Simba SC amemteua Zacharia Hans Poppe kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, huku Makamu wake akiwa ni Kassim Mohammed Dewji.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya klabu, Msimbazi, Dar es Salaam Aveva aliwataja Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa ni Said Tuliy, Musley Al Ruwaih, Crescentius Magori na Dk Roadney Chiduo.
    Rais wa Simba SC, Evans Aveva (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari

    Aveva pia ameunda Kamati mbili zaidi, ya Soka ya Vijana itakayokuwa chini ya Mwenyekiti, Said Tuliy, Ally Suru, Patrick Rweyemamu, Mulamu Nghambi, Madaraka Suleiman na Amina Poyo.
    Kamati ya Mashindano Mwenyekiti wake atakuwa Mohammed Nassor, Makamu Iddi Kajuna na Wajumbe Jerry Yambi, Hussein Simba na Mohammed Omar.      
    Aveva amesema pia baada ya kikao cha kwanza cha Kamati ya Utendaji jana, Mohammed Nassor, Musleh Al Ruwaih na Salim Abdallah wameteuliwa katika Kamati ya Utendaji.
    Aveva amesema kikao cha jana pia kiliamua kuwasimamisha uanachama, wanachama 69 waliokwenda  Mahakamani kupinga uchaguzi wa klabu hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita.
    Amesema hatima ya wanachama hao, pamoja na ya mwanachama mwingine maarufu, Michael Wambura aliyeenguliwa kwenye uchaguzi kwa kosa kama hilo, itaamuliwa katika Mkutano Mkuu Agosti 3, mwaka huu.  


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AVEVA AMTEUA DEWJI KUMSAIDIA KAZI HANS POPPE, AUNDA KAMATI ‘NZITO’ YA MASHINDANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top