CAMEROON imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kuaga Kombe la Dunia na ya pili kwa ujumla baada ya waliokuwa mabingwa watetezi, Hispania.
Hiyo inafuatia kuchapwa mabao 4-0 usiku huu na Croatia katika mchezo wa Kundi A mjini Manaus, Brazil, ambao ilimpoteza kwa kadi nyekundu kiungo wake Alex Song aliyemchezea rafu Mario Mandzukic dakika ya 40.
Cameroon imebakiza mchezo mmoja na wenyeji Brazil ikiwa haina pointi, wakati tayari Brazil na Mexico kila moja ina pointi nne na Croatia ina pointi tatu.
Punguza kasi: Danijel Pranjic akimkwatua Benjamin Moukandjo katuka mchezo huo
Brazil lazima ipate japo sare katika mchezo wa mwisho ili kujihakikishia kuingia 16 Bora- maana yake Cameroon wanaweza kurejea Younde bila ushindi.
Mabao yaliyowazamisha Simba Wasiofungika usiku huu yametiwa kimiani na Olic dakika ya 11, Perisic dakika ya 48 na Mandzukic mawili, dakika ya 61 na 73, wakati Song alitolewa dakika ya 40.
Kikosi cha Cameroon kilikuwa; Itanjde, Mbia, Chedjou/Nounkeu dk46, N’Koulou, Assou-Ekotto, Song, Matip, Enoh, Moukandjo, Aboubakar/Webo dk70 na Choupo/Salli.
Croatia; Pletikosa, Srna, Lovren, Corluka, Pranjic, Rakitic, Modric, Sammir/Kovacic dk70, Perisic/Rebic dk78, Mandzukic na Olic/Eduardo dk69.
Kiungo wa zamani wa Arsenal, Alex Song akitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Mario Mandzukic



.png)
0 comments:
Post a Comment