IMEWEKWA SEPTEMBA 1, 2013 SAA 10:55 ALFAJIRI
KLABU ya Manchester City imezinduka na kupata ushindi wa mabao 2-0 katika Ligi Kuu ya England, dhidi ya Hull City jana, Alvaro Negredo akifungua akaunti yake ya mabao katika lii hiyo.
Kocha Steve Bruce wa Hull City alionyesha kuwa na kikosi imara uwanjani ambacho kiliwanyima raha mashabiki wa Etihad, lakini kikailinika dakika ya 65 kwa bao la kichwa la Mspanyola huyo.
Baada ya kipigo cha wiki iliyopita kutoka kwa Cardiff, timu iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, vijana wa Manuel Pellegrini jana hawakutaka kurudia makosa na Yaya Toure alifuna bao la pili dakika ya 90.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Lescott, Kolarov, Nastasic, Navas, Aguero/Milner dk76, Silva/Nasri dk66, Fernandinho, Toure na Dzeko/Negredo dk46.
Hull: McGregor, Figueroa, Chester, Davies, Elmohamady, Huddlestone, Brady, Livermore, Aluko/Quinn dk70, Graham, Koren/Boyd dk75.

Ameenda hewani: Negredo akiruka kupiga mpira kichwa dhidi ya kipa wa Hull, Allan McGregor kufuna bao la kwanza

Njooni hapa: Alvaro Negredo (kushoto) akishangilia na wachezaji wenzake Jesus Navas na Pablo Zabaleta baada ya kufunga

Shuti: Toure akifunga kwa mpira wa adhabu dakika ya mwisho

Raha ya bao shangwe: Toure akishangilia baada ya kufunga
Hapa ni namna Alvaro Negredo alivyofunga bao la kwanza la Manchester City - sasa gonga hapa kupata zaidi yaliyojiri Etihad


Mshituko: Mchezaji wa Hull, Aluko akilalamika baada ya kupoteza nafasi ya kufunga

Akienda hewani: Jesus Navas akipambana na Tom Huddlestone

Kigumu: Joleon Lescott akiruka kichwa

Anakwenda na mpira: David Silva akimtoka Ahmed Elmohamady

Anaanguka: Kiungo wa Hull, Stephen Quinn akigombea mpira na Fernandinho

Wanazungumza tu: Refa Phil Dowd akizungumza na kocha wa Hull, Steve Bruce


.png)