• HABARI MPYA

    Friday, September 20, 2013

    HAYA NDIYO MAAJABU YA KING KIBADEN SIMBA SC

    Na Mahmoud Zubeiry, Mbeya, IMEWEKWA SEPTEMBA 20, 2013 SAA 2:00 ASUBUHI
    HATA kabla ya nusu msimu, tayari kocha mpya wa Simba SC, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ amempiku aliyekuwa kocha wa Simba SC kabla yake Mfaransa, Patrick Liewig kwa matokeo mazuri.
    Tangu Januari mwaka huu hadi Mei, Liewig aliiongoza Simba SC katika mechi 25, kati ya hizo akishinda mechi tisa, sare saba na kufungwa tisa.
    Hizo ni mechi zote ambazo Simba SC ilicheza chini ya Mfaransa huyo, za kirafiki na mashindano hadi anatupiwa virago.
    Mfalme wa rekodi Msimbazi; King Kibaden amedhihirisha ubora wake kwa mara nyingine Simba SC 


    REKODI KING KIBADEN SIMBA SC

    1. Simba SC 3-1 Rhino FC (Kirafiki, Katavi)
    2. Simba SC 2-1 Katavi Kombaini (Kirafiki, Katavi)
    3. Simba SC 1-0 Kahama United (Kirafiki, Kahama)
    4. Simba SC 1-1 Polisi Mara (Kirafiki, Mara)
    5. Simba SC 1-2 URA (Kirafiki, Taifa)
    6. Simba SC 0-1 Coastal (Kirafiki, Tanga)
    7. Simba SC 1-1 Polisi TZ (Kirafiki, Taifa)  
    8. Simba SC 4-1 SC Villa (Simba Day, Taifa)
    9. Simba SC 2-2 Rhino (Ligi Kuu, Tabora)
    10. Simba SC 1-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu, Arusha)
    11. Simba SC 4-3 Mafunzo (kirafiki, Taifa)
    12. Simba SC 2-1 KMKM (Kirafiki, Taifa)
    13. Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, Taifa)
    14. Simba SC 6-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    Lakini King Kibaden tangu aanze kazi Simba SC miezi mitatu iliyopita, ameiongoza timu katika mechi 14 tu na kushinda tisa sawa na Liewig, kufungwa mbili tu, huku akitoa sare tatu.
    Kati ya hizo zimo mechi nne za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, ambazo ameshinda tatu  kutoa sare moja, hivyo kuipandisha timu hiyo kileleni kwa kufikisha pointi 10, ikifuatiwa na JKT Ruvu na Ruvu Shooting zenye pointi tisa kila moja. 
    Hii inamaanisha Simba SC ilichukua uamuzi sahihi kuachana na Mfaransa huyo na kumrejea gwiji wake wa zamani, King Kibaden ambaye aling’ara na klabu hiyo kuanzia miaka ya 1960 hadi 1970.
    Sahau kuhusu matokeo mazuri ya sasa ya timu, King Kibaden ana mengi ya kujivunia ndani ya Simba, kuanzia kuwa mchezaji pekee aliyefunga mabao matatu katika mechi dhidi ya watani, Yanga mwaka 1977, Wekundu wa Msimbazi wakishinda 6-0, ushindi wa kihistoria.
    King Kibaden alikuwa mmoja wafungaji wa mabao mawili, yaliyoipeleka Simba SC Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1974 baada ya kuilaza 2-0 Hearts of Oak mjini Accra, Ghana, lingine akifunga Adamu Sabu (sasa marehemu).

    REKODI YA LIEWIG SIMBA SC

    1. Simba SC 4-2 Jamhuri (Kombe la Mapinduzi)
    2. Simba SC 1-1 Tusker FC (Kombe la Mapinduzi)
    3. Simba SC 1-1 Bandari (Kombe la Mapinduzi)
    4. Simba SC 0-1 U23 Oman (Kirafiki)
    5. Simba SC 1-3 Qaboos (Kirafiki)
    6. Simba 2-1 Ahly Sidab (Kirafiki)
    7. Simba SC 0-1 Black Leopard (Kirafiki)
    8. Simba 3-1 African Lyon (Ligi Kuu)
    9. Simba SC 1-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    10. Simba 1-1 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
    11. Simba SC 0-1 Recreativo de Libolo (Ligi ya Mabingwa)
    12. Simba 1-0 Prisons (Ligi Kuu)
    13. Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
    14. Simba SC 0-4 Recreativo de Libolo (Ligi ya Mabingwa) 
    15. Simba SC 2-1 Coastal Union (Ligi Kuu)
    16. Simba SC 1-0 CDA    (Ligi Kuu)
    17. Simba SC 4-0 Singida United (Kirafiki)
    18. Simba SC 1-1 Rhino FC (Kirafiki)
    19. Simba SC 0-1 Kagera Sugar    (Kirafiki)
    20. Simba SC 2-2 Toto Africans   (Ligi Kuu)
    21. Simba SC 1-1 Shinyanga United (Kirafiki)
    22. Simba SC 2-2 Azam FC (Ligi Kuu)
    23. Simba SC 3-1 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
    24. Simba SC 1-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    25. Simba SC 0-2 Yanga SC (Ligi Kuu)
    Patrick Liewig enzi zake Simba SC akiwa na Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Juma Kaseja

    Katika Nusu Fainali, Simba SC ilitolewa na Mehallal El Kubra ya Misri kwa penalti 3-0, baada ya sare ya jumla ya 1-1 kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake, ingawa kuna habari za kipa wa Simba, Athumani Mambosasa (sasa marehemu) kufanyiwa fujo, wakati wa upigwaji wa penalti.

    Ameshinda jumla ya mataji sita ya Ligi Kuu kama mchezaji akiwa Simba SC katika miaka ya 1965, 1966, 1973, 1976, 1977 na 1978, pamoja na ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1975.
    Na akiwa kocha, aliipa Simba SC ubingwa wa Muungano mwaka 1993 pamoja na kuifikisha Fainali ya Kombe la CAF mwaka huo, ikifungwa na Stella Abidjan ya Ivory Coast 2-0 Dar es Salaam.    
    Kwa sasa Kibaden, ndiye kocha bora wa Ligi Kuu tuzo aliyoipata kutokana na kazi yake nzuri akiwa Kagera Sugar ya Bukoba msimu uliopita, ambayo iliishawishi Simba SC kumrejea.
    Jumamosi, Kibaden ataiongoza Simba SC katika mchezo wa 15 tangu arejee Msimbazi, mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, je ataendeleza wimbi la ushindi? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HAYA NDIYO MAAJABU YA KING KIBADEN SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top