IMEWEKWA SEPTEMBA 21, 2013 SAA 3:59 USIKU
KIUNGO John Obi Mikel amefunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu ya England na kuiwezesha Chelsea kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Fulham Uwanja wa Stamford Bridge, huo ukiwa ushindi wao wa kwanza mwezi huu.
Mabao ya Oscar na Mikel kipindi cha pili yamemaliza ukame wa ushindi ndani ya mechi nne na kuendeleza rekodi ya Jose Mourinho kutofungwa nyumbani katika Ligi Kuu ndani ya mechi 63 na ushndi wa kwanza tangu wafungwe na Aston Villa.
Ushindi huo wa 2-0 unamaanisha Fulham inatimiza miaka 34 bila kushinda Stamford Bridge, Chelsea ikizinduka baada ya vipigo vya Everton na Basle.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Mikel, Schurrle/Lampard dk79, Oscar, Hazard/De Bruyne dk85, Eto’o/Torres dk64.
Fulham: Stockdale, Riether, Amorebieta, Hangeland, Richardson, Duff/Taarabt dk64, Parker, Sidwell, Kacaniklic/Tue Na Bangna dk72, Kasami/Rodallega dk85 na Bent.

Ushindi umerudi: Oscar akishangilia bao lake na wenzake

Oscar amefunga bao la kwanza leo Stamford Bridge

Bao tamu sana: John Obi Mikel akifunga bao lake la kwanza Ligi Kuu England baada ya mechi 258

Raha sana: Obi akishangilia bao lake

Raha zimerejea Darajani: Jose Mourinho akishangilia ushindi wake wa kwanza mwezi huu

Mwenye timu tabasamu latosha: Roman Abramovich akiwa jukwaani kuangalia ushindi wa timu yake

Amekosa: Darren Bent alipoteza nafasi nzuri ya kufunga wakati timu hizo hazijafungana

Maumivu: Scott Parker akichezewa rafu na Gary Cahill

Hdi chini: Steve Sidwell akimuacha chini Eden Hazard baada ya kugombea naye mpira

Mabao wapi?: Samuel Eto'o kwa mara nyingine ameshindwa kuifungia timu yake mpya

John Terry akiwania mpira wa juu

Branislav Ivanovic akipambana na Pajtim Kasami

Ramires, akipambana na Alexander Kacaniklic


.png)