IMEWEKWA SEPTEMBA 19, 2013 SAA 7:00 USIKU
MECHI nne bila ushindi. Kama Rafa Benitez angekuwa bado yupo kazini, anerushiwa mayai viza.
Jose Mourinho amepata kipigo katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa baada ya Chelsea kuchapwa mabao 2-1 nyumbani na FC Basle.
Oscar alitangulia kuwafungia The Blues dakika ya 45, lakini Salah akasawazisha dakika ya 71, kabla ya Streller kufunga la ushindi dakika ya 82 Uwanja wa Stamford Bridge.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Oscar, van Ginkel/Mikel dk75, Lampard/Ba dk76, Willian/Mata dk67, Eto'o na Hazard.
Basle: Sommer, Voser, Schar, Ivanov, Safari, Salah/Xhaka dk88, Diaz, Frei, Stocker/Ajetidk 83, Sio/Delgado dk65 na Streller.

Mkono kichwani: Frank Lampard (kushoto) akionekana mnyonge wakati Basle wanashangilia ushindi wao Stamford Bridge

Wanyonge: Gary Cahill, Oscar na John Obi Mikel wakisikitikia kipigo

Mshii wa mechi: Marco Streller (wa pili kushoto) akiifungia bao la ushindi Basle

Mkali wa vichwa: Streller (katikati kushoto) akishangilia na mfngaji mwenzake Mohamed Salah

Bao: Mohamed Salah (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake wa Basle baada ya kusawazisha

La kusawazisha: Mohamed Salah (katikati) alifunga bao zuri

Huzuni tu: Jose Mourinho amefungwa mechi ya pili tangu arejee Stamford Bridge

Ujumbe kwa kocha: Shabiki la Chelsea akipeleka ujumbe kwa kocha Mourinho kwamba Juan Mata anastahili kucheza na si kukaa benchi

Benchi: Nahodha wa klabu, John Terry alisugua benchi

Anapeperusha bendera : Oscar akishangilia baada ya kuifungia Chelsea mwishoni mwa kipindi cha kwanza

Mikogo kwa mashabiki: Kiungo Mbrazil akishangilia bao lake

Oscar anakwenda kufunga

Ashley Cole akipambana na Salah


.png)