KIUNGO Gareth Barry ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya Euro 2012, kwa sababu ya majeruhi ya nyonga, Chama cha Soka kimethibitisha.
Kiungo huyo England mwenye umri wa miaka 31, alifanyiwa vipimo mapema leo, ambavyo vimethibitisha ana maumivu makubwa.
"Ninasikitishwa sana kumpoteza Gareth," alisema kocha Roy Hodgson. "Nina uhakika ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha England baada ya Euros."
Hodgson amemuita beki wa Everton, Phil Jagielka kuchukua nafasi ya Barry.
"Kikosi cha mwisho cha England cha wachezaji watatu lazima iwe kimewasilishwa kwa ajili ya fainali hizo za Poland na Ukraine mchana wa kesho.
Barry, ambaye ameichezea tmu ya taifa mechi 50, alilazimika kutoka nje baada ya dakika 30 tu baada ya kuingia akitokea benchi katika mechi ya kirafiki na Norway mjini Oslo, Jumamosi.
Uamuzi wa Hodgson kumuita Jagielka unaweza kumfanya Phil Jones ahamie kwenye nafasi ya kiungo, ambako aliwahi kucheza wakati katika klabu yake, Manchester United mwishoni mwa msimu.
Bado wachezaji Danny Welbeck na Glen Johnson, ambao wamepona hivi karibuni maumivu ya kifundo cha mguu wanaangaliwa afya zao, na wawili hao wanatarajiwa kuwasili kambini, Watford kesho.
Scott Parker pia alikuwa majeruhi, lakini amethibitisha yuko fiti akitokea benchi dakika ya 55 katika mechi ya ushindi wa England wa 1-0 dhidi ya Norway mwishoni mwa wiki.