• HABARI MPYA

    Tuesday, May 29, 2012

    MAAJABU YA MICHEZO, MESSI ALILIMWA KADI NYEKUNDU YA MOJA KWA MOJA 2005


    Messi amewahi kupewa kadi nyekundu mwaka 2005

    WAIJUA ASILI YA MCHEZO WA DARTS?
    Inaelezwa kuwa mchezo huu ulianza katika nchi za Jumuiya ya Madola barani ulaya ambapo wanajeshi walikuwa na utaratibu wa kulenga miti kwa kutumia vishale kama sehemu ya mafunzo ya kulenga shabaha.
    Kufuatia mazoezi hayo ndipo watu wengine wakaanza kuiga na kuanzisha mchezo wa Darts.
    XX
    HII NDIYO PENATI YA KWANZA KABISA
    Penati ya kwanza kabisa kupigwa katika historia ya mchezo wa soka ilikuwa kwenye mechi kati ya Wolverhampton Wanderers dhidi ya Accrington.
    Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Molineux siku ya Septemba 14 mwaka 1891.
    Kwa mujibu wa historia hiyo mchezaji wa Wolves Billy Heath ndiye aliyeweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga penati mara baada ya kupewa mpira ili aweze kupiga.
    XXX

    MPIRA WA MEZA WAWEKA REKODI YA AJABU
    Septemba 26 mwaka 2010 pale mjini Guangzhou katika uwanja wa Guangzhou mchezo wa mpira wa meza uliweka rekodi ya aina yake baada ya kuingiza watazamaji wengi zaidi kuliko kawaida.
    Mara zote tumekuwa tukishuhudia mchezo wa soka, ngumi,tenis,  kikapu ama netiboli ikiingiza mashabiki wengi zaidi uwanjani ikilingamnishwa na michezo midogo kama darts,skwashi, mpira wa meza pamoja na mingineyo.
    Lakini hii ilikuwa ajabu kwenye mchezo wa mpira wa meza ambapo kwenye uwanja wa Guangzhou nchini China jumla ya watazamaji 1,197 waliingia kutazama mchezo huo.
    Rekodi hiyo bado inaendelea kutamba na imefanya mechi hiyo kuwa kubwa kuliko zote duniani katika michezo yote iliyochezwa ya mpira wa meza.
    XXX
    MAAJABU YA MESSI KUONYESHWA KADI NYEKUNDU
    MESSI kama tunavyofahamu ni kwamba mara nyingi amekuwa si mkorofi ndani ya dimba ikiwemo kupigana na wachezaji wenzake ama kucheza rafu za hatari.
    Hii imefanya wapenzi wengi wa soka kuzua mjadala mkali wa mabishano ambapo wapo wanaosema kwamba MESSI amewahi kupata kadi nyekundu huku wengine wakisema kuwa hana kadi nyekundu tangu aanze soka lake.
    Ukweli ni kwamba mchezaji LIONEL MESSI amewahi kuonyeshwa kadi nyekundu tena ya moja kwa moja.
    Kadi hiyo nyekundu aliipata mwaka 2005 wakati akiwa anaichezea timu ya taifa ya Argentina ya vijana wenye umri chini ya miaka 20.
    Akiwa anaichezea timu hiyo dhidi ya Hungary katika mechi ya kimataifa ya kirafiki, MESSI ambaye wakati huo alikuwa na miaka 18, alionyeshwa kadi nyekundu.
    MESSI alionyeshwa kadi hiyo katika kipindi cha pili cha mchezo wakati akijaribu kumzuia kwa mkono beki wa Hungary aliyemvuta jezi kwa nyuma wakati akielekea katika lango la Hungary.
    Katika tukio hilo MESSI ambaye alikuwa kwenye kasi ya kuelekea langoni mwa timu pinzani ghafla alijikuta akivutwa jezi na beki VILMOS VANEZAK na mara tu alipojaribu kupeleka mkono wake kwa nyuma kwa bahati mbaya ukampiga shingoni mwa beki huyo na kumuumiza, kitu ambacho kilipelekea mwamuzi kumpa kadi nyekundu.
    Mechi hiyo ilimalizika kwa timu ya vijana ya Argentina kupigwa bao 2-1.
    XXXX
    WAMJUA ALIYECHEZA MECHI NYINGI ZAIDI ENGLAND?
    Mchezaji huyo si mwingine bali ni golikipa mstaafu wa kimataifa wa Uingereza PETER SHILTON ambaye amecheza jumla ya mechi 1005 za ligi kuu ya Uingereza na kuweka rekodi ya kipekee.
    Mbali na rekodi hiyo PETER SHILTON bado anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee kuichezea timu ya taifa ya Unigereza mechi nyingi zaidi kushinda mwingine yoyote.
    Ni kwamba hadi sasa SHILTON anatamba na rekodi ya kuichezea Uingereza jumla ya mechi 125 na kwa ujumla alistaafu soka mnamo mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 47.
    Full name Peter Leslie Shilton
    Date of birth(1949-09-18) 18 September 1949 (age 62)
    Place of birth Leicester, England
    Playing position Goalkeeper
    XXXXX
    By ARONE MPANDUKA(Radio Tumaini) kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya mtandao wa Intaneti.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAAJABU YA MICHEZO, MESSI ALILIMWA KADI NYEKUNDU YA MOJA KWA MOJA 2005 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top