Monday's gossip column

IVANOVIC AITAMANI OFA YA REAL MADRID, LAKINI...

BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic, mwenye umri wa miaka 28, anavutiwa na ofa ya mabingwa wa Hispania, Real Madrid ingawa amesema anafurahi kubaki Stamford Bridge.
WAKALA wa mchezaji anayetakiwa na klabu ya Manchester City, Thiago Silva, mwenye umri wa miaka 27, amesema beki huyo anaweza kukubali kuondoka San Siro ikiwa AC Milan itataka kumuuza.
KLABU ya AC Milan inataka kumsajili mshambujliaji wa Manchester City, Carlos Tevez, mwenye umri wa miaka 28, baada ya kukwama kumsajili Muargentina huyo Januari.
Manchester United defender Michael Keane
Michael Keane has represented Republic of Ireland at youth levels
KOCHA aliyekalia kuti kavu Blackburn, Steve Kean anataka kumsajili kinda wa Manchester United, mwenye umri wa miaka 19, pacha Michael Keane kwea mkopo wakati Rovers ikijiandaa na Ligi Daraja la Kwanza.
MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero, mwenye umri wa miaka 23, kwa dau la pauni Milioni 50 anawaniwa na klabu ya Real Madrid, lakini amegoma kuhama Etihad. "Maisha yangu yapo Manchester City. Nataka kubaki hapa," alisema.
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka 24, amethibitisha yupo kwenye mazungumzo na klabu kadhaa juu ya mpango wa kuhama Emirates.

HODGDON KWENDA BRAZIL

KOCHA wa England, Roy Hodgson amejipanga sawa sawa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 ili afanye vizuri na kujitengenezea mazingira ya kuwa kocha wa muda mrefu wa timu hiyo.
KOCHA wa England, Roy Hodgson atasafiri kwenda Brazil moja kwa moja baada ya mashindano ya Euro 2012, kwenda kukagua sehemu ambayo itafaa kwa Three Lions kuweka kambi ya kujiandaa na Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini humo.
BEKI wa Fulham, raia wa Norway, Brede Hangeland, mwenye umri wa miaka 30, amesema wachezaji wa  England wanatakiwa kudhihirisha ubora wao kwenye Euro 2012, baada ya msimu mrefu wa mafanikio.
NYOTA Scott Parker, mwenye umri wa miaka 31, amezungumzia anavyojisikia vizuri baada ya kuwa fiti kwa ajili ya kuiwakilisha England kwenye Euro 2012, baada ya kuumizwa na klabu yake kukosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Tottenham player Giovani Dos Santos
Giovani Dos Santos.
KIUNGO Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 33, anakabiliwa na mkanganyiko wa mawazo kwenye Euro 2012 baada ya kocha wa  England, Roy Hodgson kuamua chaguo lake la kwanza katika safu ya kiungo ya timu ni Steven Gerrard na Scott Parker.
BEKI wa zamani wa Arsenal na Tottenham, Sol Campbell amewaonya mashabiki wa England kutokwenda kwenye fainali za Euro 2012, kwa sababu wanaweza kurejea na maumivu.
NYOTA wa Tottenham, mwanaoska wa kimataifa wa Mexico, Giovani Dos Santos, mwenye umri wa miaka 23, anaweza akaomba kuondoka, vinginevyo ahakikishiwe kuchezeshwa kwenye Uwanja wa White Hart Lane.
KLABU ya Liverpool itafanya mazungumzo na kocha wa Swansea, Brendan Rodgers katika kukamilisha msako wao wa kumtafuta mrithi wa Kenny Dalglish.
MMILIKI wa Wigan, Dave Whelan yuko tayari kutimiza masharti ya kocha Roberto Martinez, ili kumzuia asihamie Liverpool au Aston Villa.
THE Latics wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Waandishi wa Habari, ili Martinez aseme kama atapenda kubaki au kuondoka.

MUGABE CHELSEA DAMU

RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema yeye ni shabiki wa Chelsea tangu klabu hiyo ya London, itwae taji la Ligi ya Mabingw3a Ulaya kwa kuifunga Bayern Munich.