• HABARI MPYA

    Thursday, May 31, 2012

    WABUNGE WA CHADEMA WAAGWA KWA MTANANGE WA BRAZIL NA MAREKANI


    Baaada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha tawi la chadema Washington Dc Maryland na Virginia,Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mhe. Peter  Msigwa na  Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu  Dogo janja, Usiku wa Jana Jumatano Mei 30,2011  waagwa rasmi kwa kuangalia mpambano wa kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
    Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uwongozi wa tawi la Chadema Washington Dc Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry wa pili kulia, pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa. (Picha maelezo na swahilivilla.blog spot.com)

    Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mpambano huo ni 67,656 wakiwemo  Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe, Peter Msigwa.  (Picha maelezo na swahilivilla.blog spot.com)

    Wabunge wa chama cha Chadema wakipata flash ya pamoja na warembo wa Kibrazil ndani ya uwanja wa FedexField, uliopo Landover Maryland Nchini marekani. (Picha maelezo na swahilivilla.blog spot.com)

    Picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil Usiku wa kuamkia leo  Alhamis Mei 31,2012 ndani ya ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
    Nabendera ya Taifa wakishangilia Bao la  kwanza la Brazil lilifungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar
    Wachezaji wa Brazil wakilinda ngome yao kwa kuwadhibiti timu ya US kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambapo timu ya Brazil waliweza kuwabamiza US bao 4-1 nyumbani kwao.
    US. hoi kwa Brazil baada ya kubamizwa bao nne bao la kwanza lilifungwa na Neymar, na lapili na Thiago mnamo wa dakika ya 11, kipindi cha kwanza. bao la US lilifungwa na Hercules Gomes dakika ya 44 kipindi chakwanza hadi mapumziko Brazil 2 US 1 kwenye mchezo wa kirafiki. (Picha maelezo na swahilivilla.blog spot.com)
    Landon Donovan
    Forward wa United States Landon Donovan, akipandisha majeshi juu huku alidhibitiwa na Brazil defender Marcelo wa Brazi katika mpambano wa kirafiki.
    Hivyo ndivyo ilivyo katika uwanja wa FedexFeild, uliopo Landover Maryland Nchini Marekani  (Picha maelezo na swahilivilla.blog spot.com).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WABUNGE WA CHADEMA WAAGWA KWA MTANANGE WA BRAZIL NA MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top