• HABARI MPYA

    Wednesday, May 23, 2012

    JERRY SANTO, NSA JOB WATUA COASTAL UNION, MWALALA NA WASSO WATUPIWA VIRAGO

    KLABU ya Coastal Union ya Tanga, ipo mbioni kumsajili kiungo Mkenya, Jerry Santo (pichani kushoto) aliyewahi kuchezea Simba SC.
    Ofisa Habari wa klabu hiyo, Edo Kumwembe amesema mazungumzo yanaendelea juu ya mpango wa kumsajili nyota huyo, aliyecheza kwa mafanikio SImba SC
    “Tuko kwenye usajili sasa hivi, tayari tumeishawanasa wachezaji wawili na sasa tuko katika hatu ya mwisho na Jerry Santo,” alisema Edo. 
    Mapema jana, akizungumza na Habari Leo, Katibu Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siag alisema, imewaacha wachezaji wake tisa wakiwemo Ally Ahmed ‘Shiboli’, Benard Mwalala na Ramadhani Wasso,  Enock John, Laurent Mugia, Bakari Mohamed, Daudi Changula na Francis Busungu. 
    Katibu huyo alisema moja ya sababu za kuchukua uamuzi huo ni kutokana na kushuka kwa viwango vyao vya uchezaji na kwamba wana matumaini makubwa timu yao mwakani itakuwa moto wa kuotea mbali. 
    Alisema Kamati ya Usajili ya Coastal Union inaendelea na harakati za kufanya usajili wa nguvu kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi msimu ujao. 
    Aliwataja wachezaji ambao wamewasajili kuwa ni Nsa Job kutoka Villa Squad na kiungo Sudy Mohmed wa Toto Africans ya Mwanza.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JERRY SANTO, NSA JOB WATUA COASTAL UNION, MWALALA NA WASSO WATUPIWA VIRAGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top