Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya

NEWCASTLE KUMPOTEZA DEMBA BA

KLABU ya Newcastle United itajitoa mhanga kumpoteza mshambuliaji wake mkali, Demba Ba mwenye umri wa miaka 26,msimu huu kwa kugoma kujadili naye marekebisho ya mkataba wake kuondoa kipengele cha kumruhusu kwa dau la pauni Milioni 7.
KLABU ya Chelsea ilikuwa ina dau la pauni Milioni 32.4 kwa ajili ya kumnunua kiungo chipukizi wa Brazil, Lucas Moura ambalo hata hivyo lilikataliwa na rais wa klabu yake, Sao Paulo, Juvenal Juvenico. "Lucas ni mchezaji babu kubwa mwenye ubora wa hali ya juu anayeisaidia sana timu ," Juvenico alisema kuhusu kinda huyo wa umri wa miaka 19, aliyeichezea mechi 11 timu yake ya taifa.
Newcastle striker Demba Ba
Demba Ba .
KLABU ya Manchester United inaandaa mamilioni ya kutosha kwa ajili ya mpachika mabao wa Montpellier, Olivier Giroud. Sir Alex Ferguson anataka kuanza majadiliano na washindi hao wa Ligue 1 kabla ya Euro 2012, kuangali uwezekano wa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amezitupilia mbali tetesi kwamba klabu hiyo iko tayari kuwatoa washambuliaji wake Carlos Tevez au Mario Balotelli kama sehemu ya mpango wa kumpata mshambuliaji mwenye umri wa miaka 27 wa AC Milan, Thiago Silva.
MSHAMBULIAJI wa Porto, Hulk, mwenye umri wa miaka 25, anataka kuchukua nafasi ya Didier Drogba katika mshambuliaji wa akiba katika kikosi cha Chelsea. Porto imetaka kiasi kisichopungua pauni Milioni 38 kwa ajili ya mshambuliaji wao huyo, lakini Chelsea haiwezi kutoa zaidi ya pauni Milioni 30.
KLABU ya Everton tayari imempata mbadala wa Leighton Baines, beki wa kushoto ambaye anaweza kutimkia Manchester United msimu ujao. Kocha Manager David Moyes amemtambulisha beki Mfaransa, Aly Cissokho, mwenye umri wa miaka 24, kama mbadala wake, ambaye wanaweza kumnunua kwa pauni Milioni 6.
NAHODHA wa Uholanzi, Mark van Bommel amemtaka mchezaji mwenzake wa kimataifa wa timu hiyo, Arjen Robben mwenye umri wa miaka 28, kufikiria kwa uzito wa juu kuhama Bayern Munich msimu huu, baada ya kuzomewa na mashabiki wa Munich katika mechi ya kirafiki baina ya timu hizo, Bayern na Ujerumani.. Winga huyo wa zamani wa Chelsea, anaweza kuvutiwa na klabu za Manchester United na Liverpool.
KOCHA wa AC Milan amepanga kuzungumza na Liverpool Juni kuhusu kiungo wa mkopo Alberto Aquilani. Kiungo huyo wa kimataifa wa Italia, mwenye umri wa miaka 27, ameshindwa kucheza mechi kamili 25 akiwa na The Rossoneri, kiwango ambacho kinaweza kumfanya anunuliwe moja kwa moja kutoka Wekundu wa Anfield.
KLABU ya Manchester United inataka kumsajili Ezequiel Lavezzi, mshambuliaji wa Napoli kutoka Argentine mwenye umri wa miaka 27, kwa dau la pauni Milioni 25.
Habari kamili: Journal of Naples
KLABU ya Bolton ina matumaini ya kuendelea kuwa na kinda la Arsenal, Ryo Miyaichi kwa msimu mwingine katika Uwanja wa Reebok wakiwa na matumaini ya kurejea Ligi Kuu msimu ujao. Kiungo huyo wa The Gunners, mwenye umri wa miaka 19, amekuwa na msimu mzuri licha ya kwamba The Trotters wa meshuka daraja.

TORRES APEWA MKATABA WA MSHAMBULIAJI MKUU CHESLEA

BAADA ya kutishia anataka kuondoka Chelsea msimu huu, mshambuliaji wa Kispanyola, Fernando Torres amepokea fomu ya kuhakikishiwa na klabu hiyo kwamba atakuwa atakuwa mshambuliaji mkuu Stamford Bridge msimu ujao.
KOCHA wa zamani wa England, Fabio Capello, ambaye aliacha madaraka hayo February, hayumo kwenye orodha ya wamiliki wa klabu ya Liverpool katika makocha wanaotakiwa kuziba nafasi ya hiyo iliyo wazi Anfeld.
Chelsea striker Fernando Torres
Fernando Torres.

MAN CITY YAPATA HASARA BALAA


KLABU ya Manchester City imepoteza pauni Milioni 197 msimu uliopita, hasara kubwa mno ndani ya mwaka mmoja katika historia ya klabu hiyo. Klabu zote 20 za Ligi Kuu kwa ujumla zimepoteza pauni Milioni 361 mwaka jana, baada ya kutumia na kuvuka kiwango cha rekodi ya faida yao, pauni Bilioni 2.3.
KIUNGO wa zamani wa Bolton, Jay Jay Okocha anakumbuka enzi zake katika klabu hiyo, aliisaidia kuifanya Trotters kuwa moja ya timju imara katika Ligi Kuu, ingawa hiyo sasa imepotea. "Jitihada zetu zetu zimetupwa. inafikiriwa kama vile kazi yetu yote ilikuwa bure," alisema.