• HABARI MPYA

    Tuesday, May 29, 2012

    ITALIA YATAJA KIKOSI CHA MAUAJI HASWA EURO 2012, BALOTELLI NDANI


    Ranocchia and Destro miss Italy cut






    KOCHA wa Italia, Cesare Prandelli ametaja orodha ya mwisho ya wachezaji 23 kwa ajili ya UEFA EURO 2012 saa chache kabla ya mechi ya kirafiki na Luxembourg mjini Parma, huku beki Andrea Ranocchia na mshambuliaji Mattia Destro wakiwa wachezaji wa mwisho kuiacha kambi ya The Azzurri.

    Baada ya kupunguza wachezaji kutoka 32 hadi 25 jana, huku kipa Francesco Viviano, mabeki Davide Astori, Salvatore Bocchetti, Domenico Criscito na viungo Luca Cigarini, Ezequiel Schelotto na Marco Verratti akiwatema, Prandelli ametaja kikosi chake cha mwisho katika siku ya mwisho ya kuwasilisha orodha ya wachezaji kwa ajili ya michuano hiyo.

    Nyota mwenye umri wa miaka 24, Ranocchia aliyepitia msimu mgumu kwa kuandamwa na majeruhi akiwa na FC Inter Milan na kinda wa miaka 21, Destro kwa mastaajabu ya wengi wameorodheshwa kikosini. Kinda huyo, Destro amefunga mabao 12 msimu huu Serie A akiwa na AC Siena.

    KIKOSI KAMILI ITALI;
    Makipa; Gianluigi Buffon (Juventus), Morgan De Sanctis (SSC Napoli), Salvatore Sirigu (Paris Saint-Germain FC).

    Mabeki: Ignazio Abate (AC Milan), Federico Balzaretti (US Città di Palermo), Andrea Barzagli (Juventus), Leonardo Bonucci (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Christian Maggio (SSC Napoli), Angelo Ogbonna (Torino FC).

    Viungo: Daniele De Rossi (AS Roma), Alessandro Diamanti (Bologna FC), Emanuele Giaccherini (Juventus) Claudio Marchisio (Juventus), Riccardo Montolivo (ACF Fiorentina), Thiago Motta (Paris Saint-Germain FC), Antonio Nocerino (AC Milan), Andrea Pirlo (Juventus).

    Washambuliaji: Mario Balotelli (Manchester City FC), Fabio Borini (AS Roma), Antonio Cassano (AC Milan), Antonio Di Natale (Udinese Calcio), Sebastian Giovinco (FC Parma)








    Cesare Prandelli has named his final 23-man squad for the EURO©Getty Images

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ITALIA YATAJA KIKOSI CHA MAUAJI HASWA EURO 2012, BALOTELLI NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top