• HABARI MPYA

    Tuesday, May 29, 2012

    MCHAKATO MISS WORLD WAANZA RASMI TANZANIA


    Salha Israel, Miss Tanzania 2011
    KAMPUNI ya Lino International Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, imewataka warembo wanaotaka kushindana katika shindano dogo la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia (Miss World 2012) wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kushindana katika kinyang’anyiro hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 4.
    Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba sema  kuwa wanatarajia kufanya mchujo wa washiriki Juni 5 kwa ajili ya kubakiza warembo 10 kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika Agosti 18 kwenye ukumbi wa Dongsheng Fitness Center Stadium,  mjini Ordos, Inner Mongolia, China.
    Lundenga alisema kuwa  zoezi hilo lilisimamishwa kutokana na zuio la Serikali na  wakati huo, jumla ya warembo 12 walikuwa wamekwisha chukua fomu za kushiriki. Alisema kuwa muda wa kufanya mashindano hayo umekaribia na wanatarajia kuitangaza tarehe mpya hivi karibuni.
    Alisema kuwa amefurahishwa na kasi ya kuchukua na kurejesha fomu, hata hivyo wanahitaji warembo wengi zaidi ili kuweza kupata wigo mpana kwa ajili ya kumsaka mrembo atakayewania taji la Dunia ambalo kwa sasa lina mikononi mwa mrembo kutoka Venezuela, Ivian Sarcos.
    “Tunakaribia kufanya mashindano madogo hivi karibuni, hivyo ni wajibu wetu kuwakumbusha warembo wanaotaka kuwania taji hilo kufanya hivyo kabla ya Juni 4 ili kuweza kuingia katika zoezi la mchujo,” alisema Lundenga.
    Alisema kuwa mpaka sasa jumla ya nchi 84 zimekwisha pata wawakilishi wao kwa ajili ya mashindano hayo. Nchi 32 pamoja na Tanzania bado hazija chagua wawakilishi wao katika mashindano hayo.
     Fomu za kuomba kushiriki zinapatikana katika ofisi za Miss Tanzania za jijini na mawakala wote wa mashindano hayo katika mikoa ya Tanzania Bara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHAKATO MISS WORLD WAANZA RASMI TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top