• HABARI MPYA

    Thursday, April 30, 2026

    JKT TANZANIA YAICHAPA KMC 1-0 UWANJA WA MEJA ISAMUHYO


    TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Bao pekee la timu hiyo ya jeshi Kujenga Taifa limefungwa na mshambuliaji Valentino Mashaka Kusengama kwa mkwaju wa penalti dakika ya 13 ya mchezo huo.
    Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 32 na kurejea nafasi ya nne ikiizidi pointi tatu Pamba Jiji FC baada ya timu hizo zote kucheza mechi 20.
    Hali inazidi kuwa mbaya kwa KMC FC baada ya kupoteza mchezo huo ikibaki na pointi zake tisa ikiendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 kufuatia kucheza mechi 20 pia.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT TANZANIA YAICHAPA KMC 1-0 UWANJA WA MEJA ISAMUHYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top