• HABARI MPYA

    Wednesday, April 15, 2026

    COASTAL UNION YAICHAPA DODOMA JIJI 3-1 MKWAKWANI


    TIMU ya Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Mabao ya Coastal Union yamefungwa na kiungo Grayson Gwalala dakika ya 15, mshambuliaji Maabad Maulid dakika ya 32 na kiungo Geoffrey Manyasi dakika ya 90’+4, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na mshambuliaji Waziri Junior dakika ya 90’+1.
    Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya 12 kutoka ya 13, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 24 nafasi ya nane kwenye Ligi ya timu 16 baada ya timu hizo kucheza mechi 19.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA DODOMA JIJI 3-1 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top