• HABARI MPYA

    Monday, April 06, 2026

    COASTAL CHUPUCHUPU KUCHAPWA NA MTIBWA NYUMBANI, SARE 1-1 MKWAKWANI


    WENYEJI, Coastal Union wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Mtibwa Sugar walitangulia kwa bao la kiungo Geoffrey Manyasi aliyejifunga dakika ya 36, kabla ya kiungo mwingine, Cleophas Mkandala kuisawazishia Coastal Union dakika ya  80.
    Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 18 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya tisa, wakati Coastal Union inafikisha pointi 16 katika mchezo wa 18 pia ingawa inabaki nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL CHUPUCHUPU KUCHAPWA NA MTIBWA NYUMBANI, SARE 1-1 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top